Jumuiya ya Afrika Mashariki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Jumuiya ya Afrika Mashariki
Kiingereza: East African Community
Wito: Taifa Moja Mustakabali Mmoja
Kiingereza: "One People One Destiny"
Wimbo wa taifa: EAC Anthem
Makao makuu Arusha, Tanzania
Lugha rasmi Kiswahili, Kiingereza
Aina Shirika la kimataifa
Uanachama Bendera ya Burundi Burundi
Bendera ya Kenya Kenya
Bendera ya Rwanda Rwanda
 South Sudan
Bendera ya Tanzania Tanzania
Bendera ya Uganda Uganda
Viongozi
 -  Mwenyekiti John Magufuli
 -  Mwenyekiti wa Baraza Shem Bageine
 -  Rais wa Mahakama Harold Nsekela
 -  Spika wa Bunge Margaret Zziwa
 -  Katibu Mkuu Richard Sezibera
Bunge Bunge la EAC (EALA)
Maanzilisho
 -  Mara ya kwanza 1967 
 -  Kufutwa 1977 
 -  Mara ya pili 7 July 2000 
Eneo
 -  Jumla 1,820,664 km2 (17th a)
702,962 sq mi 
 -  Maji (%) 5.6
Idadi ya watu
 -  2014 makisio 153,301,178[1] a (9th)
 -  Density 84.2/km2
218.1/sq mi
Pato la Taifa makisio 2013 
 -  Total US$ 297.791 billion[2] (51sta)
 -  Per capita US$ 1942
GDP (nominal) 2013 estimate
 -  Total US$ 122.672 billion (61sta)
 -  Per capita US$ 800 a
Currency
Saa za eneo CAT / EAT (UTC+2 / +3)
Tovuti
eac.int
a. If considered as a single entity.
b. To be replaced by the East African shilling
Nchi tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki

Jumuiya ya Afrika Mashariki au Mtangamano wa Afrika Mashariki (kwa Kiingereza East African Community, kifupi EAC) ni muundo wa kisiasa unaounganisha nchi tano za kanda ya Maziwa Makuu ya Afrika Mashariki: Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda.[3] Mnamo Machi 2016 Sudan Kusini imekuwa nchi wa sita.[4]

Eneo la Mtangamano ni 1,820,664 square kilometres (702,962 sq mi), likiwa na wakazi 153,301,178[1] (kadirio la mwaka 2014)[5]

Jumuiya yenye jina hilo imepatikana mara mbili katika historia: jumuia ya nchi tatu kubwa zaidi kati ya hizo ilianzishwa mwaka 1967, lakini ilisambaratika mwaka 1977[6][7][8].

Jumuiya ilifufuliwa rasmi tarehe 7 Julai 2000.[9]

Jumuiya ya kwanza[hariri | hariri chanzo]

Nchi tano za Afrika ya Mashariki zilizokuwa chini ya utawala wa Uingereza na Ubelgiji zilianza uhuru wao kwa kuendeleza ushirikiano wa karibu uliorithiwa kutokana na utawala wa pamoja wakati wa ukoloni.

Baada ya kupata uhuru mwaka 1961 nchi tatu ziliunda Mamlaka ya Huduma za Pamoja za Afrika ya Mashariki (kwa Kiingereza East African Common Services Organisation – kifupi EACSO).

Ushirikiano ulihusu fedha (East African Shilling), forodha (Customs Union), huduma za reli (East African Railway), ndege (East African Airways), mabandari, posta na simu na elimu ya juu (Chuo Kikuu cha Afrika ya Mashariki chenye kampasi Makerere, Dar es Salaam na Nairobi). Mkataba ulilenga pia mahakama kuu ya pamoja na sera ya kiuchumi ya soko la pamoja. Haya yote yalitakiwa kuwa chini ya Bunge la Afrika ya Mashariki.

Tangu 1965 umoja huo ulianza kurudi nyuma kila nchi ilipoanzisha pesa yake.

Mwaka 1967 nchi tatu zilijaribu upya kuimarisha umoja wao kwa Mkataba wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki wakiita umoja wao "Jumuiya ya Afrika ya Mashariki" ikiwa na makao makuu Arusha, Tanzania.

Lakini mielekeo ya nchi zote tatu zilitofautiana mno: Kenya iliendelea kwa njia ya upebari lakini Tanzania ilijaribu kujenga Ujamaa (usoshalisti) kuanzia mwaka 1967. Uganda uliingia katika kipindi cha udikteta kali ya Idi Amini aliyeharibu uhusiano na majirani alipoanza kudai sehemu za maeneo yao.

Sababu nyingine ni madai ya Kenya ya kuwa na viti zaidi kuliko Uganda na Tanzania katika kamati za maamuzi,[10] huku kukiwa na kutokuelewana kulikosababishwa na udikteta wa Idi Amin nchini Uganda, Usoshalisti huko Tanzania, na soko huria nchini Kenya,[7] hivyo wanachama hawa watatu wakapoteza ushirikiano wa miaka zaidi ya sitini na manufaa ya ukubwa wa jumuiya hii kiuchumi. Kila mmoja wa wanachama hawa ilimbidi kuanza kutoa huduma na kujenga viwanda ambavyo hapo awali vilikuwa chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hivyo mwaka 1977 Jumuiya ya Afrika Mashariki ilikoma kufanya kazi yoyote na 1983 ilifutwa rasmi. Mali iliyobaki iligawanywa kati ya nchi zote tatu.

Kufufuka kwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki tangu 1993[hariri | hariri chanzo]

Tangu miaka ya 1990 majaribio ya kujenga umoja mpya yalionekana tena.

Marais Moi wa Kenya, Mwinyi wa Tanzania, na Museveni wa Uganda walipatana katika Mkataba wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki huko Arusha, tarehe 30 Novemba 1993, na kuanzisha Tume ya Ushirikiano ya nchi hizi tatu. Shughuli ya kuzileta pamoja nchi hizi kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni, utafiti na teknolojia, ulinzi, usalama, masuala ya kisheria na kimahakama ilianza.

Jumuiya mpya ya Afrika ya Mashariki ilianzishwa mnamo Januari 2001 huko Arusha penye makao makuu ya jumuiya hii.

Mkataba 2004 uliweka msingi wa Umoja wa Forodha ulioanzishwa 2005.

Kuna tena Bunge la Afrika ya Mashariki linalojumuisha wabunge waliochaguliwa na mabunge ya nchi wanachama.

Pia Mahakama Kuu ya Afrika ya Mashariki imeundwa upya.

Mwaka 2008, baada ya majadiliano na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Southern Africa Development Community, kifupi SADC) na Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (Common Market for Eastern and Southern Africa, kifupi COMESA), Mtangamano huo ulikubali nchi zote za miundo hiyo mitatu ziunde eneo pana la biashara huria. Kwa sasa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni mojawapo ya nguzo muhimu za hiyo Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika (African Economic Community, kifupi AEC).

Mwaka 2010, Mtangamano ulitangaza soko la pamoja kwa bidhaa, kazi na mitaji kati ya nchi hizo tano, kwa lengo la kuanzisha pesa ya pamoja na hatimaye Shirikisho kamili.[11]

Mwaka 2013 ulisainiwa mkataba wa kuamua kuanzisha hiyo pesa ndani ya miaka 10.[12]

Tangu tarehe 20 Februari 2015 rais wa Mtangamano huo alikuwa Jakaya Kikwete, Rais wa Tanzania hadi tarehe 5 Novemba 2015, alipomuachia nafasi John Magufuli, ambaye aliongezewa mwaka mwingine mnamo Machi 2016.

Nchi wanachama na jinsi zilivyojiunga[hariri | hariri chanzo]

Kutoka kushoto: Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Mwai Kibaki wa Kenya na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania wakati wa mkutano wao Arusha, mnamo Novemba 2006.
Rais wa Rwanda Paul Kagame katika mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka wa 2006. Rwanda ilijiunga na Jumuiya ya Afrika mashariki tarehe 1 Julai 2007

Kenya, Tanzania na Uganda zina historia ya ushirikiano tangu mwanzoni mwa karne ya 20, wakati wa ukoloni,[13] ikiwa ni pamoja na Umoja wa Forodha baina ya Kenya na Uganda mwaka 1917, Tanganyika ilijiunga mnamo mwaka 1927, katika Ubalozi wa Afrika Mashariki (1948-1961), 'East African Common Services Organisation' (1961-1967) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (1967-1977).[13]

Jumuia ambayo ilianzishwa baada ya uhuru ilidumu miaka 10 tu, lakini ilifufuliwa kwa mkataba wa tarehe 30 Novemba 1999, ulioanza kufanya kazi tarehe 7 Julai 2000, miaka 23 baada ya kifo cha ile ya kwanza.

Burundi na Rwanda, ambazo ziliwahi kuwa koloni moja na Tanzania bara kabla ya Vita vikuu vya kwanza, zilijiunga na Mtangamano tarehe 6 Julai 2009.[14]

Mara baada ya kupata uhuru mwaka 2011, Sudan Kusini iliomba kujiunga na Jumuia, lakini haikukubalika hadi Machi 2016 kutokana na hali ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Hatua kubwa ya awali katika kuanzisha Shirikisho la Afrika Mashariki ni muungano wa forodha katika mataifa husika uliotiwa saini mnamo Machi 2004 na ulioanza kutumika tarehe 1 Januari mwaka 2005. Chini ya masharti ya mkataba, Kenya, ambayo ndiyo nchi inayopata mauzo bora zaidi nje ya nchi katika kanda ya Afrika Mashariki, iliendelea kulipa ushuru kwa bidhaa zake zinazoingia nchi nyingine wanachama hadi mwaka 2010, kwa kiwango kilichopungua na wakati. Mfumo sawa wa ushuru utatumika kwa bidhaa kutoka nchi ambazo si wanachama.

Vipingamizi kuelekea shirikisho[hariri | hariri chanzo]

Kwa ujumla, mataifa wanachama kwa kiasi kikubwa wanaona neema ya Shirikisho la Afrika Mashariki, lakini utafiti usio rasmi unaonyesha kwamba Watanzania wengi (asilimia themanini ya wakazi wake) wana mtazamo hasi.[15]

Tanzania imekuwa na historia ya amani tangu kunyakua uhuru, ikilinganishwa na fujo na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoshuhudiwa katika mataifa ya Kenya, Rwanda, Burundi, na Uganda. Wakati huu Afrika Mashariki inajaribu kudumisha utulivu na mafanikio katikati ya migogoro inayoendelea katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Pembe ya Afrika na Sudan Kusini.

Pia ni kwamba Tanzania peke yake ina ardhi kubwa kuliko mataifa mengine 4 yakiunganishwa, na baadhi ya Watanzania wana hofu ya unyakuzi wa ardhi na wakazi wa sasa wa mataifa mengine wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.[16] [17] [18]

Uhaba wa ardhi ni suala nyeti katika eneo la Afrika Mashariki, hasa nchini Kenya, ambako mapigano ya wenyewe kwa wenyewe upande wa Mlima Elgon mwaka 2007 yaliwaacha zaidi ya watu 150 wamefariki na kulazimisha takriban watu wengine 60,000 kugura makazi yao.[19]

Mahakama ya Afrika Mashariki[hariri | hariri chanzo]

Mahakama ya Afrika Mashariki ndiyo mahakama inayosimamia kesi zote katika eneo hilo. Kwa sasa imo mjini Arusha, Tanzania.

Bunge la Afrika Mashariki[hariri | hariri chanzo]

Bunge la Afrika Mashariki ndicho kitengo cha kutengeneza sheria katika eneo la Afrika Mashariki. Ina wajumbe 27 ambao wote wamechaguliwa na mabunge ya nchi wanachama. Linahusika na masuala yote ambayo yanahusu Jumuiya hii kama vile kujadili bajeti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na masuala yote ya Jumuiya na kutoa mapendekezo kwa Baraza juu ya mambo wanayoyadhani muhimu kwa utekelezaji wa mkataba, kushirikiana pamoja na Bunge husika na kuanzisha kamati kwa makusudi kama vile wanavyodhani ni muhimu. Tangu uzinduzi wake mwaka 2001, bodi hii imekuwa na vikao kadhaa mjini Arusha, Kampala na Nairobi.

Pasipoti ya Afrika Mashariki[hariri | hariri chanzo]

Pasipoti ya Afrika Mashariki ilizinduliwa rasmi tarehe 1 Aprili 1999 ili kurahisisha usafiri na kuvuka mipaka ya nchi husika.[20][21] Ni halali kwa kusafiri ndani ya eneo la Afrika Mashariki (Kenya,Uganda na Tanzania) na kutoa haki ya kuingia na kukaa kwa miezi sita katika nchi yoyote na kisha unaweza ukaitumia tena.[20] Pasipoti hii inapatikana katika Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji katika miji ya Nairobi, Kampala na Dar es Salaam. Ni raia tu wa Afrika Mashariki wanaoweza kuomba pasipoti hii.[20][21] Gharama ya pasipoti hii ni dola 10 za Marekani au pesa sawa ukibadilisha kwa sarafu za nchi za Afrika mashariki.[21] Baada ya kujaza fomu za kupata pasipoti hii itachukua muda wa wiki mbili au tatu kuipata tayari kwa matumizi. Ingawa pasipoti hii ni halali tu ndani ya Afrika Mashariki, majadiliano yalifanywa ili kuwa na hati sawa za kusafiri kwa watu wote wa Afrika Mashariki.[20]

Visa Moja kwa Watalii[hariri | hariri chanzo]

African Union
Map of the African Union with Suspended States.svg

Makala hii imepangwa kwa mfululizo:
Siasa na serikali ya
the African UnionNchi zingine · Atlasi

Lilikuwa tarajio la wengi kuwa kabla ya 2006 kungekuwa na visa moja kwa watalii wote wanaozuru Afrika Mashariki, iwapo mpango huo ungeidhinishwa na mamlaka ya sekta husika chini ya Jumuiya hii. Iwapo ingekubalika basi Visa hii ingetumika kote katika ardhi ya wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Chini ya pendekezo hili Visa yoyote mpya ya Afrika Mashariki ingeweza kupokelewa kutoka ubalozi wowote katika eneo la Afrika Mashariki.

Mtandao Afrika Mashariki[hariri | hariri chanzo]

Matumizi ya wavuti katika eneo la Afrika Mashariki bado yako chini mno yakilinganishwa na mataifa yaliyostawi kiuchumi.

Eneo la Afrika Mashariki ni kituo kizuri kiuchumi huku likikadiriwa kuwa na wakazi zaidi ya milioni 150. Inakadiriwa kuwa asilimia 10 ya wakazi wa Afrika Mashariki - milioni 15 - huutumia Mtandao.

Mkakati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unasisitiza ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo kwa kuzingatia uwezo wa kijamii.

Wengi wa wakazi wa Afrika Mashariki hutumia mtandao kuangalia habari, kusoma barua pepe na kwenye mitandao mingine ya kijamii.

Hivi karibuni kumekuwa na majukwaa mengi yanayoibuka katika eneo hili kwa lengo la kuileta pamoja Afrika Mashariki.

Kasi ya mawasiliano kupitia kwa mtandao pia iko chini mno katika eneo la Afrika Mashariki, ikilinganishwa na mataifa yaliyostawi. Hii labda ni mojawapo ya vikwazo vya maendeleo ya mawasiliano ya mtandao Afrika Mashariki.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Mtangamano ungehesabiwa kama nchi moja tu, ungekuwa ya 17 duniani kwa eneo. <div class="thumb tleft" style="width: Expression error: Unrecognized punctuation character "[".px; ">

Lake Victoria
Ziwa Victoria kati ya nchi za Mtangamano.
Mount Kilimanjaro
Mlima Kilimanjaro, mrefu kuliko yote ya Afrika, uko Tanzania.

Sudan Kusini, Uganda, Rwanda na Burundi hazina pwani baharini, lakini zina mvua za kutosha.

Huku inapatikana minne kati ya milima mirefu zaidi barani Afrika: Mlima Kilimanjaro (Tanzania), Mlima Kenya (Kenya), milima ya Rwenzori (Uganda/DRC) na Mlima Meru (Tanzania).

Ziwa Turkana, Kenya, ndiyo ziwa la jangwani kubwa na lenye maji ya chumvi nyingi kuliko yote duniani.

Ziwa Victoria linaunganisha nchi za Kenya, Uganda na Tanzania na ni la pili duniani kwa eneo.

Ziwa Tanganyika mashariki kwa Tanzania ni la pili duniani kwa kina.

Kenya pekee ina jangwa, jangwa la Chalbi katika Kaunti ya Marsabit.

<div class="thumb tright" style="width: Expression error: Unrecognized punctuation character "[".px; ">

Wildebeest#Migration
Uhamaji wa wanyamapori ni ajabu la kimaumbile la 7 duniani
Mount Kilimanjaro
Ziwa Nakuru, maarufu kwa flamingo.
Rosette (botany)
Dar es Salaam, ukiwa na watu milioni 4 ndio mji mkubwa kuliko yote ya Mtangamano.
Nairobi, kitovu cha biashara cha Mtangamano

Mikoa na Majimbo ya Jumuia ya Afrika Mashariki 1. Arusha 2. Dar es Salaam 3. Dodoma 3. Geita 4. Iringa 5. Kagera 6. Katavi 7. Kigoma 8. Kilimanjaro 9. Lindi 10. Manyara 11. Mara 12. Mbeya 13. Morogoro 14. Mtwara 15. Mwanza 16. Njiombe 17. Pemba Kaskazini 18. Pemba Kusini 19. Pwani 20. Rukwa 21. Ruvuma 22. Shinyanga 23. Simiyu 24. Singida 25. Songwe 26. Tabora 27. Tanga 28. Unguja Kaskazini 29. Unguja Mjini Magharibi 30. Unguja Kusini 31. Bubanza 32. Bujumbura Mairie 33. Bujumbura Rural 34. Bururi 35. Cankuzo 36. Cibitoke 37. Gitega 38. Karuzi 39. Kayanza 40. Kirundo 41. Makamba 42. Muramvya 43. Muyinga 44. Mwaro 45. Ngozi 46. Rutana 47; Ruyigi 48. Mkoa wa Kati 49. Mkoa wa Pwani 50. Mkoa wa Mashariki 51. Nairobi (Jimbo la Kati) 52. Mkoa wa Kaskazini Mashariki 53. Mkoa wa Nyanza 54. Mkoa wa Bonde la Ufa 55. Mkoa wa Magharibi 56. Gabiro 57. Kitala 58. Mkoa wa Kaskazini 59. Buganda 60. Elgon

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Jumla ya wakazi wote ilikuwa 153,301,178 mnamo Julai 2014. Hivyo ingeshika nafasi ya 9 duniani ingehesabika kama nchi moja tu.

Katika Mtangamano, hasa nchini Tanzania, zinapatikana jamii zote za makabila ya Afrika kusini kwa Sahara: Khoisan, Wakushi, Wabantu, Wanailoti.

Asilimia ya wakazi wanaoishi mijini ni 19.26% tu, lakini wanaongekeza kwa 4.71% kila mwaka.

Nchi Wakazi GDP (PPP)
(Bilioni za $US)
GDP (Nominal)
(Bilioni za $US)
Wenye elimu ya msingi (%)
1. Bendera ya Burundi Burundi &0000000010395931.00000010,395,931 7.884 2.723 67.2
2. Bendera ya Kenya Kenya &0000000045010056.00000045,010,056 125.77 56.3 87.4
3. Bendera ya Rwanda Rwanda &0000000012337138.00000012,337,138 17.362 7.431 71.1
4. Bendera ya Tanzania Tanzania &0000000049639138.00000049,639,138 84.884 33.285 67.8
5. Bendera ya Uganda Uganda &0000000035918915.00000035,918,915 61.891 22.926 73.2
Mtangamano mzima &0000000153301178.000000153,301,178 297.791 122.672 73.34

Lugha kubwa zaidi katika Mtangamano ni Kiswahili, ambacho kutoka pwani ya Kenya na Tanzania kimeenea katika nchi zote tano na nje yake pia. Lugha rasmi ni Kiingereza pia. Lugha nyingine muhimu ni kama vile Kirundi na Kinyarwanda, ingawa Kifaransa kimeenea pia.

Upande wa dini, unaongoza Ukristo (76.04%), ukifuatwa na Uislamu (14.06%) na dini asilia za Kiafrika (3.9%). Kati ya Wakristo, Wakatoliki wanaongoza nchini Burundi, kumbe Waprotestanti wanaongoza Kenya, huku aina hizo mbili zikilingana Tanzania, Uganda na Rwanda.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

 1. 1.0 1.1 https://www.cia.gov/library/publications/the-world-factbook/rankorder/2119rank.html?countryname=Kenya&countrycode=ke&regionCode=afr&rank=31#ke
 2. [1]
 3. Joint Communiqué of the eighth Summit of EAC Heads of State
 4. "South Sudan admitted into EAC", Daily Nation, 2 March 2016, reprinted at nation.co.ke, accessed 4 March 2016
 5. East African Community Facts and Figures – 2009
 6. – Born in anonymity. Ms.dk. Iliwekwa mnamo 2010-07-01.
 7. 7.0 7.1 East African trade zone off to creaky start, Christian Science Monitor, 9 Machi 2006
 8. We Celebrated at EAC Collapse, Says Njonjo.
 9. East African Community – Quick Facts. Eac.int. Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-03-19. Iliwekwa mnamo 2010-07-01.
 10. [18] ^ ms.dk - Born in anonymity
 11. "FACTBOX-East African common market begins", 1 July 2010. Retrieved on 1 July 2010. 
 12. "East African trade bloc approves monetary union deal", Reuters, 30 November 2013. 
 13. 13.0 13.1 From Co-operation to Community. Jalada kutoka ya awali juu ya 2008-05-10. Cite error: Invalid <ref> tag; name "EacSite" defined multiple times with different content
 14. EAC Update E-newsletter. www.eac.int. Directorate of Corporate Communications and Public Affairs. Iliwekwa mnamo 10 December 2011.
 15. allAfrica.com: Tanzania: Fast-Tracking Political Federation
 16. EAC federation fears justified? Tanzania's Daily News On Saturday; 5 Mei 2007
 17. Kenya: Tears for Mt Elgon as Schools Re-Open
 18. Sabiny Demand Land as Karamajong Raid Reduce
 19. AlertNet Kenya land clashes kill 60, displace thousands
 20. 20.0 20.1 20.2 20.3 EAC News ...
 21. 21.0 21.1 21.2 Travelling in East Africa

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: