Kaunti ya Tharaka-Nithi
Jump to navigation
Jump to search
Kaunti ya Tharaka-Nithi | |||
---|---|---|---|
Kaunti | |||
| |||
Tharaka-Nithi County in Kenya.svg![]() Kaunti ya Tharaka-Nithi katika Kenya | |||
Nchi | ![]() | ||
Namba | 13 | ||
Ilianzishwa | Tarehe 4 Machi, 2013 | ||
Ilitanguliwa na | Mkoa wa Mashariki | ||
Makao Makuu | Kathwana | ||
Kikao cha Serikali | Chuka | ||
Gavana | Muthomi Njuki | ||
Naibu wa Gavana | ENG. Francis Nyamu Kagwima | ||
Seneta | Kithure Kindiki | ||
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa) | Beatrice Nkatha Nyaga | ||
Bunge la Kaunti | Bunge la Kaunti ya Tharaka Nithi | ||
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa | 15 | ||
Maeneo bunge/Kaunti ndogo | 3 | ||
Eneo | 2,409.5 km2 (930.3 sq mi) | ||
Idadi ya watu | 365,330 | ||
Kanda muda | Saa za Afrika Mashariki (UTC+3) | ||
Tovuti | tharakanithi.go.ke |
Kaunti ya Tharaka-Nithi ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.
Serikali huketi Chuka, ingawa makao makuu rasmi ni Kathwana.
Jiografia[hariri | hariri chanzo]
Kaunti ya Tharaka Nithi imepakana na kaunti za Meru, Embu, Kirinyaga, Nyeri na Kitui. Ina sehemu ya Msitu wa Mlima Kenya katika upande wa magharibi. Mto Tana hupitia katika kaunti hii. Mito inayotiririsha maji ndani ya Mto Tana na hupitia Tharaka Nithi kutoka Mlima Kenya ni: Mto Mutonga, Mto Thingithu, Mto Kathita, Mto Thanantu, Mto Thangatha, Mto Kithinu and Mto Ura[1].
Utawala[hariri | hariri chanzo]
Kaunti ya Tharaka Nithi imegawanywa katika maeneo yafuatayo:
Eneo bunge | Wadi |
---|---|
Maara | Mitheru, Muthambi, Mwimbi, Ganga, Chogoria |
Chuka/Igamba-ngo'mbe | Mariani, Karingani, Magumoni, Mugwe, Igambang’ombe |
Tharaka | Gatunga, Mukothima, Nkondi, Chiakariga, Marimanti |
Tazama pia[hariri | hariri chanzo]
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- ↑ About - County Government of Tharaka Nithi. Iliwekwa mnamo 2018-04-15.
Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]
- Overview of Tharaka Nithi County Archived Februari 12, 2019 at the Wayback Machine.
![]() | Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kaunti ya Tharaka-Nithi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |