Nenda kwa yaliyomo

Kaunti ya Tana River

Majiranukta: 1°30′S 40°0′E / 1.500°S 40.000°E / -1.500; 40.000
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kaunti ya Tana River
Kaunti
Tana River County in Kenya.svg
Kaunti ya Tana River katika Kenya
Coordinates: 1°30′S 40°0′E / 1.500°S 40.000°E / -1.500; 40.000
Nchi Kenya
Namba4
IlianzishwaTarehe 4 Machi, 2013
Ilitanguliwa naMkoa wa Pwani
Makao MakuuHola
Miji mingineMadogo
GavanaDhadho Gaddae Godhana
Naibu wa GavanaKea Batuyu Salim
SenetaGolich Juma Wario
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa)Rehema Hassan
Bunge la KauntiBunge la Kaunti ya Tana River
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa15
Maeneo bunge/Kaunti ndogo3
Eneokm2 39 950.5 (sq mi 15 425.0)
Idadi ya watu893,681[1].
Wiani wa idadi ya watu8
Kanda mudaSaa za Afrika Mashariki (UTC+3)
Tovutitanariver.go.ke

Kaunti ya Tana River ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.

Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 893,681 katika eneo la km2 39,950.5, msongamano ukiwa hivyo wa watu 8 kwa kilometa mraba[2]. Kabila kuu ni Wasomali (pamoja na Wawardey, ambao kwa asili ni Waoromo) halafu Wapokomo, ambao wengi ni wakulima, na Waorma, ambao hutegemea ufugaji wa kuhamahama.

Mji wa Hola ndio makao makuu ya serikali ya kaunti na ndio mji mkubwa zaidi.

Jina lake limetokana na Mto Tana.

Kwa jumla, kaunti hiyo ni kavu na huwa na ukame. Mvua si za hakika, msimu wa mvua huja miezi za Machi-Mei na Oktoba-Desemba. Kumekuwa na migogoro kati ya wakulima na wafugaji wahamaji juu ya maji. Mafuriko pia ni tatizo la kawaida, yakisababishwa na mvua nzito katika maeneo ya juu ya Mto Tana.

Kaunti ya Tana inajumuisha maeneo kadhaa ya misitu, vichaka na mapori ambayo ni maeneo madogo ya makazi. Misitu huteuliwa kama Hifadhi ya Kitaifa ikiwa ina zaidi ya aina nne za mimea mikuu na zaidi ya aina saba za wanyama wakubwa (IUCN, 2003).

Licha ya udhahiri wa maliasili ya kutosha, eneo hili bado limetengwa katika maeneo mengine ya nchi. Juhudi za maendeleo daima huzunguka eneo kubwa la Mto Tana, licha ya kutokuweko kwa mafanikio katika miradi ya awali ya kunyunyisha maji katika wilaya, yaani, miradi za kunyunyishia maji za Bura, Hola na mradi wa kukuza mpunga wa Tana delta ambao haukufanikiwa baada ya kuharibiwa na maji ya mvua za El Nino mwaka wa 1998.

Utafiti ulioandaliwa na ALMRP, Wilaya ya Mto Tana na kukabidhiwa kwa Kamati ya Maendeleo ya Wilaya ya Tana River (2004), iligundua kuwa kaunti hiyo ilikuwa na 79% ukosefu wa chakula na huku kiwango cha umaskini kikifika hadi 62% [3].

Kaunti ya Tana River imegawiwa katika maeneo bunge na kata kama ifuatavyo:

Eneo Bunge Kata
Garsen Kipini Mashariki, Garsen Kusini, Kipini Magharibi, Garsen ya Kati, Garsen Magharibi, Garsen Kaskazini
Galole Kinakomba, Mikinduni, Chewani, Wayu
Bura Chewele, Hirimani, Bangale, Sala, Madogo

Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [4]

[hariri | hariri chanzo]
  • Tana North 110,640
  • Tana Delta 116,757
  • Tana River 88,546

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. www.knbs.or.ke
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
  3. Interim Poverty Strategy Paper (I-PSP), 2000-2003, Kenya
  4. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.