Nanyuki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Nanyuki
Maduka kando ya mtaa mkuu.
Maduka kando ya mtaa mkuu.
Maduka kando ya mtaa mkuu.
Nanyuki is located in Kenya
Nanyuki
Nanyuki

Mahali pa mji wa Nanyuki katika Kenya

Majiranukta: 0°01′0″N 37°04′0″E / 0.01667°N 37.06667°E / 0.01667; 37.06667
Nchi Kenya
Kaunti Laikipia
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 49,233

Nanyuki (kutoka Kimaasai "enkare nanyokie": mto mwekundu au sisisi wa damu) ni mji mdogo katikati ya Kenya, chini ya Mlima Kenya, mwishoni kwa reli. Nanyuki ni kata ya kaunti ya Laikipia, eneo bunge la Laikipia Mashariki[1].

Mstari wa ikweta unapita katika eneo la mji na Nanyuki ni kituo cha jeshi la anga la Kenya.

Msingi wake umewekwa mwaka 1907 na walowezi Waingereza, ambao dhuria wao bado wanaishi mjini na katika mazingira yake. Sasa Nanyuki ni kituo kikuu cha Jeshi la Anga la Kenya. Jeshi la Uingereza linatunza kituo hicho na linaendesha mazoezi kila mwaka mlimani na kwa maeneo kame kaskazini.

Nanyuki ilikuwa na idadi ya watu ya 49,233 mwaka 2009 ([2]).

Wakazi wengi huchuma fedha yao kwa kufanya biashara. Maduka mjini hugawia mashamba, ranchi na hifadhi za wanyama katika mazingira mapana. Kwanza maduka mengi yalimilikiwa na Wahindi ambao bado ni kipande kikubwa kiasi cha wakazi. Wakwezi na wabebashanta hutembelea Nanyuki wakienda na kutoka Mlima Kenya kwa njia za Sirimon na Burguret, na watalii wengi wengine hupitia mji. Kwa hiyo Nanyuki una hoteli nyingi ambazo mwingoni mwao kuna Mount Kenya Safari Club, Sportsman’s Arms Hotel, Lion’s Court, Equatorial Hotel, Mount Kenya Paradise Hotel na Joskaki Hotel. Mgahawa wa zamani sana ni Marina ambao bado unapendwa kiasi. Miaka kadhaa iliyopita mgahawa mwingine umefunguliwa kusini kwa Nanyuki ambao umejengwa ndani ya mti mkubwa sana. Unaitwa Trout Tree Restaurant na mvuto mkuu wake ni trauti apikwaye kwa namna mbalimbali. Wateja wanaweza kutembelea pia msimiko wa kufuga trauti chini ya mti.

Hakuna viwanda vikubwa katika Nanyuki. Zamani kiwanda cha nguo kilikuwako, Nanyuki Textile Mills. Uongozi wa Kiingereza umepunguka polepole na kiwanda kimefilisika mwaka 1978. Baada ya miaka kiwanda, ambacho kimebaki kizima kwa kadiri, kimenunuliwa na mkazi Mhindi wa Nanyuki. Nguo kiasi inatengenezwa sasa. Pia vilikuwako viwanda vya kupasulia mbao katika Nanyuki. Lakini vimefungika sasa au vinapata riziki kwa shida sana, kwa sababu kukata miti Mlimani Kenya kumepigiwa marufuku takriban kabisa.

Bustani iko kati ya mji na mito miwili, Nanyuki na Liki, inapitia. Ikweta inapitia sehemu ya kusini ya mji. Ukifika Nanyuki barabarani A2 kutoka upande wa kusini unaivuka. Mahali hapa panapendwa sana na watalii ambao wanapigiana picha pale. Kwa kawaida kuna wananchi wanaowaonyesha watalii athari ya kani ya Coriolis. Wanasema kwamba kani hii inasababisha maji yatokayo shimo kuzunguka upande wa kisaa au kinyume saa ukiwa kwa nusudunia ya kaskazini au ya kusini, lakini ni danganyo tu (tazama Coriolis force).

Nanyuki unafikika kwa barabara na kwa ndege. Uwanja wa ndege uko km 6.5 kusini kwa mji na unapokea ndege ndogo. Ziko huduma za ndege za Air Kenya zinazofaa wafanyabiashara na watalii kwa sababu ya hali mbaya ya barabara kutoka Nairobi. Watalii wanaweza kutembelea hifadhi kadhaa katika ujirani wa Nanyuki, kama Mount Kenya National Park, Sweetwaters Game Reserve, Lewa Wildlife Conservancy, Samburu National Reserve na Shaba National Reserve.

Maji ya mfereji katika Nanyuki ni baina ya maji safi kabisa katika Kenya, kwa sababu yanatoka mto wa Mlima Kenya. Maji yajiri kwa mifereji chini ya ufadhili wa uvutano kutoka mwanzo mpaka mafereji ya maji machafu.

Taasisi za taaluma ni Nanyuki High School, Brickwoods High School, Nanyuki Primary School, Nkando Primary School k.y.k. Makao makuu ya Kenayodemo (ushirikisho wa vijana na waari) yako mjini hapa.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Electoral Commission of Kenya: Registered voters per polling station by electoral area/ward and constituency Archived Septemba 29, 2007, at the Wayback Machine
  2. Sensa ya Kenya 2009 Archived 9 Januari 2019 at the Wayback Machine., tovuti ya KNBS, ilitazamwa Januari 2009.