Nairobi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Nairobi
Mji wa Nairobi
Mji wa Nairobi

Bendera

Nembo
Nairobi is located in Kenya
Nairobi
Nairobi
Mji wa Nairobi (Kenya)
Anwani ya kijiografia: 1°17′S 36°49′E / 1.283°S 36.817°E / -1.283; 36.817
Nchi Bendera ya Kenya Kenya
Kaunti Nairobi
Idadi ya wakazi (2009)
 - 3,138,295
Tovuti: nairobi.go.ke
Jomo Kenyatta

Nairobi ni mji mkuu wa Kenya na vilevile mojawapo ya mikoa ya Kenya. Ni kati ya miji mikubwa ya Africa ukiwa na wakazi wapatao milioni 3. Kulingana na sensa ya 2009, Nairobi ina wakaaji 3,138,295 katika eneo la 696 km2 (269 sq mi). Pamoja na votongoji vyake, Nairobi ni mji wa 12 kwa ukubwa barani Africa Jina Nairobi limetokana na neno la Kimaasai, Enkarenairobi, linalomaanisha "mahali penye maji baridi."

Lugha zote za Kenya huzungumzwa Nairobi lakini hasa ni Kiingereza na Kiswahili, pamoja na Sheng.

Eneo lake, hali ya hewa[hariri | hariri chanzo]

Nairobi imeanzishwa mahali ambako nchi tambarare ya Athi inakutana na mtelemko wa nyanda za juu zinazoongozana na Bonde la Ufa. Kitovu cha Nairobi iko zipatao 1624 m juu ya UB. Mahali pake ni kama 150 km kusini mwa ekweta. Hali ya hewa haina joto kali. Halijoto ya wastani ni 20,5° mwezi wa Machi, na 16,8° mwezi wa Julai. Mvua nyingi hunyesha mwezi wa Machi (199 mm), kiangazi ina 14mm tu wakati wa Julai.

Mitaa ya Nairobi[hariri | hariri chanzo]

Ndani ya jiji la Nairobi kuna mitaa mbalimbali kama vile Dandora, Eastleigh, Embakasi, Highridge, Huruma, Jericho, Karen, Kariobangi, Kiambiu, Kibera, Langata, Lavington, Mathare, Parklands, South C, Westlands, Kawangware Karen

Historia ya Nairobi[hariri | hariri chanzo]

Nairobi imeanzishwa mw. 1899 na Waingereza kama kambi ya kujenga Reli ya Uganda. Mahali ilikuwa karibu katikati ya Mombasa na Kampala, palikuwa na maji ikaonekana ilifaa kwa kituo njiani. Mwanzo wa Nairobi ilikuwa kambi kubwa ya hema na ghala za vifaa vya kujenga reli. Mwanzoni viongozi wengine walitaka kuacha eneo hili kwa sababu ya matope mengi. Lakini makao iliendelea kukua nyumba za mawe zikajengwa. Mw. 1905 Waingereza walihamisha ofisi kuu ya serikali yao ya kikoloni kutoka Mombasa kwenda Nairobi ikawa makao makuu ya Afrika ya Mashariki ya Kiingereza (British East Africa war, baadaye Kenya Colony).

1963 ikawa mji mkuu wa nchi huru ya Kenya.

Ikaendelea kukua haraka.

Nairobi ya leo[hariri | hariri chanzo]

Nairobi imeibuka kuwa mojawapo ya miji mikubwa katika bara la Africa. Mashirika mengi makubwa duniani yamefungua ofisi zao zinazoshuhudia eneo la Afrika ya Mashariki na Afrika ya Kati. Mojawapo ya mashirika haya ni ofisi za ya tawi la Umoja wa Mataifa (United Nations), UNEP. Kunazo pia ofisi za mabalozi wa nchi mbali mbali duniani. Nairobi, kama miji mingi mikubwa, ina matatizo mengi yanayotokea kwa sababu ya ukubwa wake. Watamaduni walioupanga mji wa nairobi hawakutegemea kuwa ungenenepa hivyo. Wataalamu wengi wametoa maoonyo mengi kuhusu ukubwa wa mji huu na uwezo wake wa kuwahudumia waakaazi wote ambao wanazidi kuongezeka kila mwaka. Nairobi imewavutia waakaazi wengi wote wakiwa na hamu ya kujitafutia riziki yao. Ijapokuwa kunao wanaofanikiwa, wengi wao hujipata wameangulia patupu wakawachwa bila pesa au hali ya kujikimu. Jambo hili limepelekea kuwepo kwa wakaazi wa maeneo yasiyotengwa wananchi, maarufu kama 'slums' kwa kimombo. Eneo kubwa zaidi jijini Nairobi ni Kibera. Eneo hili lina ukubwa wa kilomita 2 kwa 2 na wakaazi takribani milioni moja. Eneo hili halina mipango yeyote ya kuruhusu binadamu kuishi lakini umaskini umewavutia wengi kuishi kule.

Kunayo pia matatizo ya ujambazi wa kibinafsi, ujambazi wa nyumba na utekaji nyara wa magari. Matatizo haya yamesababisha watu wengi kutoupendelea mji wa Nairobi.

        Mwaka         Wakazi
1906 11.500
1911 14.000
1921 24.300
1926 29.900
1929 32.900
1931 47.800
1939 61.300
1944 108.900
1948 119.000
1955 186.000
        Mwaka         Wakazi
1957 221.700
1960 251.000
1962 266.800
1965 380.000
1969 509.300
1979 827.775
1989 1.324.570
1995 1.810.000
1999 2.143.254
2005 2.750.561
2009 3.138.369
Picha ya Nairobi, kutoka pande ya Westlands

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: