Kaunti ya Meru

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Kuhusu makao makuu, tazama Meru

Kaunti ya Meru
Kaunti
Waterbuck - Meru National Park, Kenya - 2014.JPG
Flag of Meru County.png Coat of Arms of Meru County.png
Bendera Nembo ya Serikali
Meru County in Kenya.svgMeru County in Kenya.svg
Kaunti ya Meru katika Kenya
Coordinates: 0°3′N 37°38′E / 0.050°N 37.633°E / 0.050; 37.633Coordinates: 0°3′N 37°38′E / 0.050°N 37.633°E / 0.050; 37.633
NchiFlag of Kenya.svg Kenya
Namba12
IlianzishwaTarehe 4 Machi, 2013
Ilitanguliwa naMkoa wa Mashariki
Makao MakuuMeru
Miji mingineMaua, Nkubu
GavanaKiraitu Murungi, EGH
Naibu wa GavanaTitus Ntuchiu Mutea
SenetaMithika Linturi
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa)Kawira Mwangaza
Bunge la KauntiBunge la Kaunti ya Meru
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa45
MahakamaMahakama ya Rufaa, Meru
Maeneo bunge/Kaunti ndogo9
Eneo6,930.1 km2 (2,675.7 sq mi)
Idadi ya watu1,356,301
Kanda mudaSaa za Afrika Mashariki (UTC+3)
Tovutimeru.go.ke

Kaunti ya Meru ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.

Jina lake limetokana na Wameru ambao ndio jamii kubwa zaidi katika kaunti hii.

Sehemu kubwa ya Meru ina ardhi ya rutuba na mvua ya kutosha. Ni kaunti inayojulikana kwa ukuzaji wa miraa, kama zao la biashara. Hata hivyo, ukulima wa ndizi, mahindi, majani ya chai na maharagwe hufanywa[1][2].

Makao makuu yako Meru.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Kaunti ya Meru inapakana na Kaunti za Nyeri, Laikipia, Tharaka Nithi, Isiolo na Kitui. Iko katika upande wa mashariki mwa Mlima Kenya. Sehemu ya Mbuga ya Kitaifa ya Mlima Kenya iko katika Meru. Mvua yenye kufaa pamoja na udongo wa volkano huwezesha ukulima. Sehemu za Imenti zilizo karibu na Mlima Kenya huwa ni baridi kidogo na zenye vilima. Sehemu za Tigania hazina hali zenye kufaa ukulima isipokuwa karibu na Vilima vya Nyambene, ambapo huwa baridi kidogo. Mbuga ya Kitaifa ya Meru iko katika sehemu za Igembe, kaskazini mashariki mwa kaunti[3].

Mito, k.v. Mto Kathita hutoka Mlima Kenya na Vilima vya Nyambene hutiririsha maji yake ndani ya Mto Tana[4].

Utawala[hariri | hariri chanzo]

Kaunti ya Meru imegawanywa katika maeneo yafuatayo:

Eneo bunge Wadi
Igembe Kusini Maua, Kegoi/Antubochiu, Athiru, Gaiti, Akachiu, Kanuni
Igembe Kati Akirang’ondu, Athiru, Ruujine, Igembe East Njia, Kangeta
Igembe Kaskazini Antuambui, Ntunene, Antubetwe Kiongo, Naathui, Amwathi
Tigania Magharibi Athwana, Akithi, Kianjai, Nkomo, Mbeu
Tigania Mashariki Thangatha, Mikinduri, Kiguchwa, Mithara, Karama
Imenti Kaskazini Municipality, ntima East, Ntima West, Nyaki West, Nyaki East
Buuri Timau, Kisima, Kiirua/Naari, Ruiri/Rwarera
Imenti ya Kati Mwanganthia, Abothuguchi Central, Abothuguchi West, Kiagu, Kibirichia
Imenti Kusini Mitunguu, Igoji East, Igoji West, Abogeta East, Abogeta West, Nkuene

Meru ni sehemu ya kati ya uliokuwa Mkoa wa Mashariki nchini Kenya upende wa mashariki-kaskazini wa mlima Kenya.

Eneo la Meru lilijumlishwa hadi 1992 katika wilaya ya Meru iliyogawiwa baadaye kuwa wilaya zifuatazo:

 • Meru Kati (majimbo ya uchaguzi wa South Imenti, Central Imenti, North Imenti)
 • Meru Kaskazini iliyogawiwa tena kuwa wilaya za
  • Tigania
  • Nyambene (majimbo ya uchaguzi Tigania East, Igembe, Tigania West na Ntonyiri)
 • Meru Kusini (jimbo la uchaguzi laitwa Nithi)
 • Tharaka

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. Kaunti ya Meru: Kilimo cha ndizi kimeizolea sifa - MAKALA - swahilihub.com. Iliwekwa mnamo 2018-04-14.[dead link]
 2. Ripoti ya makadrio ya mvua kuu ya 2016, Kaunti ya Meru (Kaskazini). Iliwekwa mnamo 2018-04-14.
 3. DEVELOPING A SUITABILITY MODEL FOR OPTIMIZED CROPS PRODUCTION. Iliwekwa mnamo 2018-04-14.
 4. TOPO-SEQUENCE ANALYSIS OF CLIMATE VARIABILITY AND LAND USE CHANGES AMONG SMALLHOLDER FARMERS IN MERU COUNTY, KENYA. Iliwekwa mnamo 2018-04-14.