Kaunti ya Murang'a

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kuhusu mji, soma Murang'a
Kaunti ya Murang'a
Kaunti
Muranga County Office.jpg
Bunge la Kaunti ya Murang'a
Coat of Arms of Muranga County.png
Nembo ya Serikali
Murang’a County in Kenya.svgMurang’a County in Kenya.svg
Kaunti ya Murang'a katika Kenya
NchiFlag of Kenya.svg Kenya
Namba21
IlianzishwaTarehe 4 Machi, 2013
Ilitanguliwa naMkoa wa Kati
Makao MakuuMurang'a
Miji mingineMaragua, Kangema
GavanaMwangi wa Iria
Naibu wa GavanaJames Kamau Maina
SenetaIrungu Kang’ata
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa)Sabina Wanjiru Chege
Bunge la KauntiBunge la Kaunti ya Murang'a
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa35
Maeneo bunge/Kaunti ndogo7
Eneo2,325.8 km2 (898.0 sq mi)
Idadi ya watu942,581
Kanda mudaSaa za Afrika Mashariki (UTC+3)
Tovutimurang'a.go.ke

Kaunti ya Murang'a ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.

Makao makuu yako Murang'a.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Reli

Kaunti ya Murang'a imepakana na Nyeri (kaskazini), Embu, Machakos (mashariki), Kiambu (kusini) na Nyandarua (magharibi).

Kaunti hii iko kati ya m 914 na m 3353 juu ya usawa wa bahari wastani. Sehemu za magharibi zimekaribia Milima Aberdare na hivyo kuinuka zaidi. Ina mito kadhaa inayotiririka kutoka vitako vya Milima Aberdare kuelekea magharibi ambapo hutiririsha maji katika Mto Tana[1].

Murang'a ina vilima na mabonde ambayo huwezesha mito kutiririka. Topografia hii huwa na madhara wakati wa mvua kubwa kwa sababu ya mporomoko wa ardhi[2].

Udongo wa kaunti hii ni wa volkano ambao una rutuba inayowezesha kilimo. Murang'a huhusika katika kilimo cha kahawa, chai, ng'ombe wa maziwa na miti kama zao la biashara[1].

Murang'a ina maeneo matatu ya tabianchi[1]:

  • Msitu wa mvua wa tropiki, magharibi karibu na Milima Aberdare
  • Nusutropiki, maeneo ya kati
  • Nusuyabisi, mashariki

Utawala[hariri | hariri chanzo]

Kaunti ya Murang'a imegawanywa katika maeneo yafuatayo:

Eneo bunge/kata ndogo Wadi
Kangema Kanyenya-Ini, Muguru, Rwathia
Mathioya Gitugi, Kiru, Kamacharia
Kiharu Wangu, Mugoiri, Mbiri, Township, Murarandia, Gaturi
Kigumo Kahumbu, Muthithi, Kigumo, Kangari, Kinyona
Maragwa Kimorori/Wempa, Makuyu, Kambiti, Kamahuhu, Ichagaki, Nginda
Kandara Ng'araria, Muruka, Kagundu-Ini, Gaichanjiru, Ithiru, Ruchu
Gatanga Ithanga, Kakuzi/Mitubiri, Mugumo-Ini, Kihumbu-Ini, Gatanga, Kariara

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 FIRST COUNTY INTEGRATED DEVELOPMENT PLAN 2013-2017[dead link], iliwekwa mnamo 10-05-2018
  2. OCCURENCE OF LANDSLIDES WITHIN MURANG'A COUNTY. Iliwekwa mnamo 2018-05-01.[dead link]