Kaunti ya Marsabit

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kaunti ya Marsabit
Kaunti
Marsabit-County-Headquarters.jpg
Makao Makuu ya serikali ya Kaunti ya Marsabit
Flag of Marsabit County.png Coat of Arms of Marsabit County.png
Bendera Nembo ya Serikali
Marsabit County in Kenya.svgMarsabit County in Kenya.svg
Kaunti ya Marsabit katika Kenya
Coordinates: 2°19′N 37°58′E / 2.317°N 37.967°E / 2.317; 37.967Coordinates: 2°19′N 37°58′E / 2.317°N 37.967°E / 2.317; 37.967
NchiFlag of Kenya.svg Kenya
Namba10
IlianzishwaTarehe 4 Machi, 2013
Ilitanguliwa naMkoa wa Mashariki
Makao MakuuMarsabit
Miji mingineMoyale, Sololo
GavanaMohsmuf Mohamed Ali
Naibu wa GavanaSolomon Gubo Riwe
SenetaGodana Hargura
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa)Safia Sheikh Adan
Bunge la KauntiBunge la Kaunti ya Marsabit
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa20
Maeneo bunge/Kaunti ndogo4
Eneo66,923.1 km2 (25,839.2 sq mi)
Idadi ya watu291,166
Kanda mudaSaa za Afrika Mashariki (UTC+3)
Tovutimarsabit.go.ke

Kaunti ya Marsabit ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.

Makao makuu yako Marsabit. Mji mkubwa zaidi ni Moyale ulio katika mpaka wa Kenya na Uhabeshi.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Kaunti ya marsabit ni kavu. Ina Jangwa la Chalbi ambalo ni jangwa kweli la pekee katika Kenya. Kaunti za Marsabit, Turkana na Samburu hushiriki Ziwa Turkana. Mbuga ya Kitaifa ya Sibiloi hupatikana katika fuo za Ziwa Turkana katika upande wa Marsabit. Hifadhi ya Kitaifa ya Losai hupatikana katika mpaka wa Kaunti ya Marsabit na Samburu. Mlima Marsabit uko katika Hifadhi ya Kitaifa ya Marsabit. Mlima Kulal na Vilima vya Huri hupatikana katika kaunti hii[1].

Utawala[hariri | hariri chanzo]

Kaunti ya marsabit imegawanywa kaunti ndogo zifuatazo[2]:

Kaunti ndogo/Eneo bunge Wadi
Moyale Butiye, Sololo, Heillu/Manyatta, Golbo, Moyale Township, Uran, Obbu
North Horr Dukana, Maikona, Turbi, North Horr, Illeret
Saku Sagate/Jaldesa, Karare, Marsabit Central
Laisamis Loiyangalani, Kargi/South Horr, Korr/Ngurunit, Logo Logo, Laisamis

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. SAMMY WAWERU, "IJUE KAUNTI YA MARSABIT[dead link]", SwahiliHub, ilipatikana 13-04-2018
  2. "Kuhusu Marsabit", Serikali ya Marsabit, ilipatikana 13-04-2018