Nenda kwa yaliyomo

Eldama Ravine

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Eldama Ravine


Eldama Ravine
Kaunti Baringo
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 45,799

Eldama Ravine ni mji wa Kenya, kaunti ya Baringo, katika Bonde la Ufa la Afrika Mashariki.

Wakazi walikuwa 45,799 wakati wa sensa ya mwaka 2009[1].

Maeneo yenye watu wengi ni nyanda za juu kama maji mazuri, timboroa, torongo na viunga vya mji wenyewe. Nyanda za chini ni kame na yana watu wachache.

Eneo hili lina misitu ya asili pamoja na inayopandwa. Eneo Chemususu lina eneo kubwa zaidi yenya miti ya asili. Maeneo mengine yana misitu za kupandwa yenye mita kama Cypress, Pine na Eucalyptus, maeneo haya ni Sabatia, Timboroa, Maji Mazuri na Esageri.

Mazao ni mahindi, viazi vyekundu, machungwa, mboga na matunda mbalimbali.

  1. Sensa ya Kenya 2009 Archived 9 Januari 2019 at the Wayback Machine., tovuti ya KNBS, ilitazamwa Januari 2009.