Kaunti ya Kiambu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kuhusu mji, soma Kiambu
Kaunti ya Kiambu
Kaunti
Kenya 2013. Rift Valley. Viewpoint. - panoramio (1).jpg
Bonde la Ufa katika barabara kuu ya Nairobi-Nakuru, Lari
Flag of Kiambu County.svg
Bendera
Kiambu County in Kenya.svgKiambu County in Kenya.svg
Kaunti ya Kiambu katika Kenya
NchiFlag of Kenya.svg Kenya
IlianzishwaMachi 4th 2013
Ilitanguliwa naMkoa wa Kati
Makao MakuuKiambu
Kikao cha SerikaliThika
GavanaFerdinand Waititu
Naibu wa GavanaDkt. James Nyoro
SenetaKimani Wamatangi
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa)Gathoni wa Muchomba
Bunge la KauntiBunge la Kaunti ya Kiambu
SpikaStephen Ndichu[1]
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa60[2]
Maeneo bunge/Kaunti ndogo12
Eneo2,449.2 km2 (945.6 sq mi)
Idadi ya watu1,623,282[3]
Kanda mudaSaa za Afrika Mashariki (UTC+3)
Tovutikiambu.go.ke

Kaunti ya Kiambu ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.

Ilikuwa mojawapo ya wilaya za Kenya katika Mkoa wa Kati baada ya nchi kupata uhuru.

Makao makuu ya kaunti hii ni mji wa Kiambu. Hata hivyo, utendaji wa kaunti hutekeleza majukumu yake kutoka Thika.

Kupakana na Nairobi kumeifanya iwe na idadi ya wakazi wengi mijini, kwa sababu ya maendeleo katika sekta ya mali yasiyohamishika. Sekta za viwanda na ukulima pia zimechangia kukuza kaunti hii kiuchumi.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Kaunti hii imepakana na kaunti za Nairobi (kusini), Machakos (mashariki), Nakuru (magharibi), Nyandarua (kaskazini magharibi) na Murang'a (kaskazini).

Topografia ya kaunti ina nyanda za juu na nyanda za kati.

  1. Nyanda za juu kabisa zinapatikana katika kata ndogo ya Lari, ambazo ni kuenea kwa Safu za Nyandarua. Sehemu hiyo huwa na vilima vikali na ni chanzo cha maji.
  2. Nyanda za juu wastani ziko katika Limuru na sehemu za Gatundu Kusini, Gatundu Kaskazini, Githunguri na Kabete. Sehemu hizo zina vilima na tambarare zilizoinuka.
  3. Nyanda za kati hupatikana katika Juja, Thika na Ruiru. Sehemu hizo huwa kavu kidogo kuliko sehemu zingine za kaunti[4].

Kaunti ina vyanzo kadhaa vya maji.

Kiambu hupata misimu miwili ya mvua: Machi hadi Mei na Septemba hadi Disemba. Miezi kati ya Juni hadi Agosti huwa msimu wa baridi kali. Halijoto hutegemea na eneo. Maeneo ya nyanda za juu hupata baridi zaidi. Kata ndogo za Lari na Limuru na sehemu za magharibi za Gatundu Kusini, Gatundu Kaskazini na Githunguri hupata ukungu mzito na baridi ifikayo 7°c[4].

Serikali na Utawala[hariri | hariri chanzo]

Utendaji[hariri | hariri chanzo]

Gavana, sasa Ferdinand Waititu, ndiye mkuu wa kaunti na serikali. Yeye huchaguliwa kwa muhula wa miaka mitano katika uchaguzi mkuu. Ana nguvu za utendaji na za kuteua wanakamati wa Kamati ya Utendaji ya Kaunti baada ya kuidhinishwa na Bunge la Kaunti. Hata ingawa mji mkuu wa kaunti uko Kiambu, utendaji wa serikali uko mji wa Thika.

Bunge[hariri | hariri chanzo]

Bunge la Kaunti ya Kiambu ni la chumba kimoja. Lina wajumbe 60 waliochaguliwa kutoka wadi sitini za kaunti na wajumbe 27 walioteuliwa[5]. Kila mjumbe anashikilia hatamu ya miaka mitano, inayofanywa upya katika uchaguzi mkuu. Spika wa bunge na naibu wake huchaguliwa na wajumbe. Bunge la Kiambu liko katika mji wa Kiambu.

Mahakama[hariri | hariri chanzo]

Kuna Mahakama Kuu ya Kiambu iliyoanzishwa tarehe 20 Juni 2016. Ina jaji mmoja.[6]

Utawala[hariri | hariri chanzo]

Kamishna wa kaunti huteuliwa na Rais wa Kenya. Yeye ni mwakilishi wa rais kusaidia na mambo ya utawala wa serikali ya kitaifa.

Kaunti ndogo[hariri | hariri chanzo]

Kaunti imegawanywa katika maeneo yafuatayo:

Eneo bunge/kata ndogo Wadi
Githunguri Githunguri, Githiga, Ikinu, Ngewa, Komothai 3
Kiambaa Cianda, Karuri, Ndenderu, Muchatha, Kihara
Kabete Gitaru, Muguga, Nyathuna, Kabete, Uthiru
Limuru Bibirioni, Limuru Kati, Ndeiya, Limuru Mashariki, Ngecha Tigoni
Lari Kinale, Kijabe, Nyanduma, Kamburu, Lari/Kirenga
Gatundu Kaskazini Gituamba, Githobokoni, Chania, Mang'u
Gatundu Kusini Kiamwangi, Kiganjo, Ndarugo, Ng'enda
Ruiru Githothua, Biashara, Gatongora, Kahawa Sukari, Kahawa Wendani, Kiuu, Mwiki, Mwihoko 1
Kikuyu Karai, Nachu, Sigona, Kikuyu, Kinoo
Juja Murera, Theta, Juja, Witeithie, Kalimoni
Thika Township, Kamenu, Hospital, Gatuanyaga
Kiambu Ting'ang'a, Ndumberi 3, Riabai, Township

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]