Wikipedia:Matukio ya hivi karibuni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

45,000[hariri chanzo]

Tarehe 12 Agosti 2018 makala ya 45,000 imetungwa kuhusu mto Ilangi, korongo wa Kenya. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:11, 12 Agosti 2018 (UTC)

44,000[hariri chanzo]

Tarehe 30 Julai 2018 makala ya 44,000 imetungwa kuhusu mto Nyairoko. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:55, 30 Julai 2018 (UTC)

43,000[hariri chanzo]

Tarehe 7 Julai makala ya 43,000 imetungwa kuhusu mto Kaptarit. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:36, 7 Julai 2018 (UTC)

42,000[hariri chanzo]

Tarehe 21 Mei 2018, makala ya 42,000 imetungwa kuhusu mto Jigulu. Mbele kwa mbele! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:18, 21 Mei 2018 (UTC)

41,000[hariri chanzo]

Tarehe 2 Mei 2018, makala ya 41,000 ilianzishwa na Ndugu Riccardo kuhusu Mto Ligunga. Tusonge mbeleee! --Baba Tabita (majadiliano) 05:13, 3 Mei 2018 (UTC)

Ninja Ndugu Riccardo katika ubora wake. Safi sana! Tunasonga. Sasa hivi tutafika walipo Afrikaans!--Muddyb Mwanaharakati Longa 08:22, 3 Mei 2018 (UTC)

40,000[hariri chanzo]

Tarehe 17 Machi 2018, makala ya 40,000 (AROBAINI ELFU, jamani!) ni kuhusu mlima Nidze. Makala ilianzishwa na Ndugu Riccardo. Asante na hongera, Mzee! Sherehe itafanyika wapiii? Tupo pamoja katika furaha na fahari. --Baba Tabita (majadiliano) 09:52, 17 Machi 2018 (UTC)

Sasa niseme tu, zama zangu zimeisha! Nyakati zangu nilipiga buku ndani ya wiki 2. Furaha iliyopo hadi mgonjwa umeamka kitandani. Pole sana mzee wangu, Oliver, na ahsante kwa taarifa!--MwanaharakatiLonga 12:37, 17 Machi 2018 (UTC)
Kweli tunahitaji sherehe. Hongereni ndugu zangu wote! --Ndesanjo (majadiliano) 23:44, 30 Mei 2018 (UTC)

39,000[hariri chanzo]

Tarehe 24 Desemba 2017, makala ya 39,000 imeandikwa. Sasa tunalenga ya 40,000: tujitahidi pamoja. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:48, 13 Januari 2018 (UTC)

38,000[hariri chanzo]

Tarehe 12 Oktoba 2017, makala ya 38,000 ni kuhusu Ziwa Kamnarok, ziwa lililokauka la Kenya. Makala iliandikwa na Ndugu Riccardo. --Baba Tabita (majadiliano) 21:16, 13 Oktoba 2017 (UTC)

37,000[hariri chanzo]

Tarehe 30 Julai 2017, makala ya 37,000 ni kuhusu Ziwa Ambussel, ziwa dogo la Tanzania. Makala iliandikwa na Ndugu Riccardo. --Baba Tabita (majadiliano) 17:44, 30 Julai 2017 (UTC)

36,000[hariri chanzo]

Tarehe 20 Mei 2017, makala ya 36,000 ni kuhusu Abdallah Majurah Bulembo, mwanasiasa wa Tanzania. Makala iliandikwa na Ndugu Luhazi. --Baba Tabita (majadiliano) 18:29, 20 Mei 2017 (UTC)

35,000[hariri chanzo]

Tarehe 12 Januari 2017, makala ya 35,000 ni kuhusu mwandishi James Tate aliyepokea Tuzo ya Pulitzer ya Ushairi mwaka wa 1992. --Baba Tabita (majadiliano) 10:41, 12 Januari 2017 (UTC)

33,000[hariri chanzo]

18 Aprili 2016, makala ya 33,000 ni Kio'du, lugha ya Vietnam na Laos. --Baba Tabita (majadiliano) 11:43, 18 Aprili 2016 (UTC)

Warsha ya Wikipedia Morogoro[hariri chanzo]

Tarehe 21 Machi 2015, wahariri wafuatao walitoa warsha ya kuandika na kuhariri makala za wikipedia ya Kiswahili kwa walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari ya AlfaGems mjini Morogoro: Riccardo Riccioni, Kipala, ChriKo na Baba Tabita (bahati mbaya, Muddyb Blast Producer alibanwa kazini na kutoweza kuhudhuria). Tumefurahi kuona mafanikio mema!

30,000[hariri chanzo]

Nimejitahidi lakini nahisi aliyepita ni Riccardo mnamo tar. 21. Septemba 2015, sina uhakika makala gani. Kipala (majadiliano) 21:32, 23 Septemba 2015 (UTC)

Ni Historia ya Madagaska tarehe 22 Septemba 2015. Hongera kwa wote! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:55, 24 Septemba 2015 (UTC)

29,000[hariri chanzo]

 • 13 Juni 2015, makala ya 29,000 ni Pembe kuu‎ (pembe ya 180°, isiyoonekana kama pembe inafanana na mstari wa kawaida...)

28,000[hariri chanzo]

22,000[hariri chanzo]

 • 28-Oktoba-2011 imefika makala 22,000!

20,000[hariri chanzo]

Wikipedia 20000 articles.png

15,000[hariri chanzo]

 • 25 Desemba 2009 (UTC) :-)

Mlimba ni tarafa iliyopo katika wilaya ya Kilombero katika Mkoa wa Morogoro. Ipo umbali wa kilomita 150 kutoka Ifakara mjini. Tarafa ya Mlimba ina ujumla wa kata 6. Kata ya Tanganyika Masagati ni kata maarufu sana katika tarafa ya Mlimba. Ipo umbali usiopungua kilomita 100 kutoka Mlimba mjini. Tarafa hii inakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo ya usafiri, utumishi wa umma {walimu,madaktari n.k}. Wakazi wa mlimba wanategemea zaidi usafiri wa TAZARA. Kata ya Mlimba ina shule za msingi zisizopungua 10 na sekondari 3.Tarafa ya Mlimba ina shule zaidi ya 30 za msingi na 8 za sekondari. Moja kati ya shule maarufu ni shule ya msingi MAKIRIKA na shule ya sekondari MLIMBA GIRLS. Shule ya msingi MAKIRIKA ipo umbali wa kilomita 10 kutoka Mlimba mjini. Shule hii ipo katika kijiji cha Makirika. Ina walimu 4 {Donatus Dacky, Abel Michael, John Justine na Selemani Mkonje},shule ina darasa la awali hadi la saba! Pia katika tarafa ya mlimba utakutana na mgodi wa umeme{KIHANSI}... imehaririwa na selemani mkonje

Maendeleo ya makala za kata nchini Tanzania[hariri chanzo]

Makala za kata zinafuata majina ya kata yaliyotajwa katika taarifa ya sensa 2002. Kata zilizoanzishwa baadaye kwa kawaida hazipo bado. Kata zote za Tanzania zimepata makala fupi ya mbegu; mengine yameshapanushwa. Ilikuwa kazi kubwa na ya maana!

Kazi inayobaki ni kufuatilia habari za wilaya mpya zilizoanzishwa mwaka 2006/2007 kwa sababu orodha ya kata iliyopatikana ilikuwa ya sensa ya mwaka 2002. Pale tulipotambua wilaya mpya tulianza makala ya wilaya pia kigezo cha kata zake isipokuwa bado bila majina. Kata ya wilaya mpya bado zinaorodheshwa chini ya chini ya wilaya mama. Mifano ya wilaya mpya ni Wilaya ya Misenyi, Wilaya ya Chato, Wilaya ya Rorya.

Mikoa ya Tanzania ambayo kata zote zimeanzishwa makala ya mbegu[hariri chanzo]

Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Iringa | Kagera | Kilimanjaro | Kigoma | Lindi | Mara | Mwanza | Mbeya | Manyara | Morogoro | Mtwara | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Singida | Tabora | Tanga | Unguja Mjini Magharibi | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini

Wikipedia yetu katika orodha ya meta:List of Wikipedias by edits per article[hariri chanzo]

Meta:List_of_Wikipedias_by_sample_of_articles inalinganisha wikipedia za lugha mbalimbali kwenye msingi wa orodha la Makala za msingi za kamusi elezo.

Katika ulinganisho wa Aprili 2009 makala zifuatazo ziliangaliwa hasa kuwa ama zinekosekana kabisa au ni fupi mno au ziko na ukubwa karibu na ngazi inayofuata (kati ya ndogo-wastani-kubwa na kila ngazi inapewa uzito tofauti katika ulinganisho).

Majina yafuatayo ni katika wikipedia ya Kiingereza.

 1. Song (wimbo - alama 463 pekee)
 2. Crusades - vita za misalaba
 3. Communism - ukomunisti
 4. Culture - utamaduni
 5. Bang Big Bang - mlipuko mkuu
 6. Evolution - mageuko ya spishi
 7. Democracy - demokrasia
 8. Horse - farasi
 9. Basketball - mpira wa kikapu
 10. Fashism - ufashisti

--Kipala (majadiliano) 17:21, 9 Aprili 2009 (UTC)

Mradi mpya: Wilaya, tarafa na kata za Kenya[hariri chanzo]

Baada ya kutunga makala za mbegu kwa kila kata ya Tanzania tunalenga sasa kufanya kazi hiyohiyo kwa kata zote za Kenya. Ukurasa Wilaya, tarafa na kata za Kenya umeundwa kwa muda kwa kurahisisha utekelezaji wa mradi huu. Orodha hii inafikiwa pia kwa kifupikata Kenya.

Swahili Wikipedia now the largest African language Wikipedia[hariri chanzo]

Apologies for the English, I don't speak Swahili, but I thought I'd let everyone know that Swahili has just passed Afrikaans as the largest African language Wikipedia. Congratulations! See greenman.co.za for more information. Greenman (majadiliano) 22:12, 3 Agosti 2009 (UTC)