Algeria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
الجمهورية الجزائرية الديمقراطية الشعبية
Al-Jumhurīyah al-Jazā’irīyah ad-Dīmuqrāṭīyah ash-Sha’bīyah
ⵟⴰⴳⴷⵓⴷⴰ ⵜⴰⵎⴻⴳⴷⴰⵢⵜ ⵜⴰⵖⴻⵔⴼⴰⵏⵜ ⵜⴰⵣⵣⴰⵢⵔⵉⵜ
Bendera ya Algeria Nembo ya Algeria
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Kiarabu: من الشعب و للشعب


(IPA transliteration: aθ-θawratu mina-ʃ-ʃaʕbi wa-li-ʃ-ʃaʕb
(Translation: "Mapinduzi ya watu kwa ajili ya watu")

Wimbo wa taifa: Kassaman (qasaman bin-nāzilāt il-māḥiqāt)
(Arabic: Twayamini kwa radi inayoharibu)
Lokeshen ya Algeria
Mji mkuu Algiers [1]
36°42′ N 3°13′ E
Mji mkubwa nchini Algiers
Lugha rasmi Kiarabu, Kiberber
Serikali Demokrasia Jamhuri
Abdelmadjid Tebboune
Abdelaziz Djerad
Uhuru
Tarehe
kutoka Ufaransa
5 Julai 1962 [2]
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
2,381,741 km² (10th)
kidogo sana
Idadi ya watu
 - 2015 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
39,500,000 [1] (ya 35)
{{{population_density}}}/km² (ya 208)
Fedha Dinari ya Algeria (DZD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
CET (UTC+1)
CET (UTC(hawajali))
Intaneti TLD .dz
Kodi ya simu +213

-Algeria (pia: Aljeria; kwa Kiarabu: الجزائر al-Jazā’ir; kwa Kiberber: Dzayer, ⴷⵣⴰⵢⴻⵔ; kwa jina rasmi "Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Algeria") ni nchi ya Afrika ya Kaskazini-Magharibi. Imepakana na bahari ya Mediteranea, Moroko, Sahara ya Magharibi, Mauretania, Mali, Niger, Libya na Tunisia.

Ramani ya Algeria.

Algeria ni nchi kubwa kuliko zote za Afrika lakini sehemu kubwa ya eneo lake iko katika jangwa la Sahara.

Jina la nchi limetokana na mji mkuu unaoitwa kwa jina lilelile "al-jaza-ir" kama nchi ya leo kwa lugha ya Kiarabu.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Sehemu kubwa ya nchi ni jangwa, Sahara iko upande wa kusini. Asilimia 20 za eneo la Algeria upande wa kaskazini ni makao kwa karibu wakazi wote. Maeneo haya ni pwani ya Mediteranea na milima ya Atlas.

Atlas inapanda hadi kimo cha mita 2,308 juu ya UB.

Sahara inaanza kusini kwa Atlas na kanda yenye nyasi chache, halafu inafuata eneo la matuta ya mchanga pasipo mimea yote. Kusini kwake tena ni nyanda za juu ambazo ni hasa maeneo ya miamba mitupu.

Kusini kabisa kuna milima kama Tassili n'Ajjer na Ahaggar inayopanda hadi mita 2,918 na kuwa kama visiwa vya uoto katika jangwa.

Mito ya kudumu iko kaskazini tu, sehemu za pwani. Mabonde ya mito ya ndani ni makavu, isipokuwa baada ya mvua mito mikali inajitokeza kwa masaa kadhaa.

Hali ya hewa[hariri | hariri chanzo]

Kanda la kaskazini lina hali ya hewa inayoathiriwa na Bahari ya Mediteranea. Huko halijoto kwenye mwezi Agosti ni 25 °C na 12 °C wakati wa Januari.

Kwenye sehemu za juu kuna baridi na hata barafu kwenye majira ya Januari lakini joto ni kali zaidi wakati wa Julai/Agosti.

Kusini ya Atlas inaanza hali ya hewa ya jangwani; halijoto inaweza kucheza zaidi ya 20 °C katika siku moja. Wakati wa joto halijoto inapita 40 °C lakini wakati wa baridi halijoto inashuka chini ya °C kwenye saa za usiku.

Mvua ni haba mno: kuna miaka mfululizo bila tone hata moja. Katika milima ya Ahaggar kuna usimbishaji kidogo kutokana na ukungu, kwa hiyo miti kadhaa na mimea mingine iko.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Historia ya kale[hariri | hariri chanzo]

Historia inayojulikana ilianza na Waberber ambao wametokana na mchanganyiko wa wakazi asilia.

Tangu mwaka 1000 KK Wafinisia walianza kufika na kujenga miji yao ya biashara kwenye pwani ya Mediteranea. Muhimu zaidi kati ya miji yao ulikuwa Karthago uliopanua utawala wake hadi Hispania na Gallia (Ufaransa ya Kusini).

Kumbe Waberber wa bara walijenga milki zao za Numidia na Mauretania.

Katika vita kati ya Karthago na Roma ya Kale Waberber walisimama upande wa Roma, hivyo wakapata uhuru wao kwa muda kidogo, lakini wakati wa karne ya 1 KK Roma ilianza kutawala eneo la Algeria moja kwa moja.

Numidia na Mauretania zilikuwa mashamba ya Roma na sehemu kubwa ya nafaka za Italia zililimwa huko.

Mawe ya maghofu ya miji ya kale bado yanaonyesha uhusiano wa Algeria na Dola la Roma lililoitawala kwa karne nyingi hadi kuja kwa Waarabu katikati ya karne ya 7.

Utawala wa Roma ulivurugika baada ya Wavandali kutoka Ulaya Kaskazini kufika na kuanzisha milki yao kwa muda wa karne moja.

Jeshi la Kaisari Justiniani I wa Bizanti ilirudisha utawala wa Kiroma, ila tu katika karne ya 7 uvamizi wa Waarabu Waislamu ulimaliza kipindi cha Kiroma.

Uvamizi wa Waarabu[hariri | hariri chanzo]

Kuanzia mwaka 642 vikosi vya Waislamu Waarabu kutoka Misri walishambulia eneo la Afrika ya Kaskazini. Mwanzoni hawakufaulu kuwashinda Wabizanti lakini, baada ya uhamisho wa serikali ya makhalifa kutoka Medina kwenda Dameski, Waumawiya walikaza jitihada huko Afrika ya kaskazini.

Mwaka 670 jeshi kubwa la Waarabu likaunda mji wa Kairuan kusini ya Tunis ya leo na mji huu ulikuwa kitovu cha uenezaji. Walipoenea katika Algeria ya leo walirudishwa na Waberber Wakristo kwa msaada wa Wabizanti lakini jeshi lililofuata lilishinda na kufikia mwaka 711 Afrika ya kaskazini yote (maana yake nchi za leo za Tunisia, Algeria na Moroko) zilikuwa chini ya utawala wa Waarabu. Hapo sehemu kubwa ya Waberber walifanya haraka kujiunga na Uislamu wakasaidiana na Waarabu.

Matokeo hayo yalikuwa chanzo cha mabadiliko makubwa ya kudumu, maana yake upanuzi wa lugha ya Kiarabu kati ya wananchi na uenezaji wa Uislamu.

Ukoloni wa Wafaransa[hariri | hariri chanzo]

Historia ya karibuni imeacha kumbukumbu yake inayoonekana katika athira kubwa ya lugha na utamaduni wa Kifaransa kutokana na ukoloni wa Ufaransa kati ya miaka 1830 na 1962.

Kwa Marais wa nchi tangu uhuru, angalia Orodha ya Marais wa Algeria.

Kwa sasa Algeria inajenga upya umoja wa kitaifa baada ya vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyoishia mwaka 2002.

Nchi imebaki na idadi kubwa (25-30%) ya wakazi wa kabila la Waberber ambao kihistoria ndio wakazi asilia. Lakini kwa lugha, utamaduni na historia Algeria ya leo ni sehemu ya dunia ya Kiarabu.

Wilaya za Aljeria[hariri | hariri chanzo]

Kuna vitengo vya utawala 48 vinavyoitwa wilaya, zinazolingana zaidi na mikoa katika nchi zingine.


1 Adrar
2 Chlef
3 Laghouat
4 Oum el-Bouaghi
5 Batna
6 Béjaïa
7 Biskra
8 Béchar
9 Blida
10 Bouira
11 Tamanghasset
12 Tébessa


13 Tlemcen
14 Tiaret
15 Tizi Ouzou
16 Algiers
17 Djelfa
18 Jijel
19 Sétif
20 Saida
21 Skikda
22 Sidi Bel Abbes
23 Annaba
24 Guelma


25 Constantine
26 Médéa
27 Mostaganem
28 M'Sila
29 Mascara
30 Ouargla
31 Oran
32 El Bayadh
33 Illizi
34 Bordj Bou Arréridj
35 Boumerdès
36 El Tarf


37 Tindouf
38 Tissemsilt
39 El Oued
40 Khenchela
41 Souk Ahras
42 Tipasa
43 Mila
44 Aïn Defla
45 Naama
46 Aïn Témouchent
47 Ghardaïa
48 Relizane

Miji[hariri | hariri chanzo]

Watu[hariri | hariri chanzo]

Wakazi wengi wana mchanganyiko wa damu ya Kiarabu na ya Kiberber na wachache ya Kituruki na ya Kiberber; karibu wote (98%) wanafuata dini ya Uislamu.

Wakristo ni 1%, wakiwemo Waprotestanti na Wakatoliki, lakini wengine wanashindwa kujitokeza kutokana na hofu ya dhuluma.

Lugha rasmi ni Kiarabu (72%) na Kiberber (27-30%), lakini wengi sana wanaongea pia Kifaransa.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 CIA World Factbook Algeria (accessed 4 Aprili 2006)
  2. Algeria County analysis Energy Information Administration (accessed 4 Aprili 2006)

Kujisomea[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Serikali
Maelezo zaidi


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
Makala hii kuhusu maeneo ya Algeria bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Algeria kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.