Roma
Mji wa Roma | |||
| |||
Majiranukta: 41°53′N 12°30′E / 41.883°N 12.500°E | |||
Nchi | Italia | ||
---|---|---|---|
Mkoa | Lazio | ||
Idadi ya wakazi (2018) | |||
- Wakazi kwa ujumla | 2.860.009 | ||
Tovuti: www.comune.roma.it |
Roma (pia Rumi) ni mji mkuu ("Roma Capitale") wa Jamhuri ya Italia. Pia ni mji mkuu wa mkoa wa Lazio.
Roma iko katika sehemu ya magharibi ya kati ya Rasi ya Italia, katika makutano ya mito ya Tiber na Aniene karibu na Bahari ya Mediteranea.
Roma ina wakazi 2,860,009 katika 1,285 km2 (496.1 sq mi),[1] Roma ni komune yenye watu wengi zaidi nchini na ni jiji la tatu lenye watu wengi katika Umoja wa Ulaya kwa idadi ya watu ndani ya mipaka ya jiji.
Roma mara nyingi inajulikana kama Jiji la Milima Saba kutokana na eneo lake la kijiografia, na pia kama "Mji wa Milele". Roma kwa ujumla inachukuliwa kuwa "chimbuko la ustaarabu wa magharibi na Utamaduni wa Kikristo", na kitovu cha Kanisa Katoliki.[2][3][4] Mji wa Vatikano[5] (nchi ndogo zaidi duniani) ni nchi huru ndani ya mipaka ya jiji la Roma, mfano pekee uliopo wa nchi ndani ya jiji.
Eneo la Roma
[hariri | hariri chanzo]Roma uko katikati ya Italia ikiwa mita 20 juu ya UB ndani ya tambarare ya bonde la mto Tiber linalopakana na milima ya Abruzzi, milima ya Sabini na milima ya Albani.
Wilaya za jirani ni Viterbo, Rieti, L'Aquila, Frosinone na Latina.
Mwanzo wa Roma ulikuwa kwenye vilima saba vilivyo katikati ya mji wa leo vinavyoitwa: Palatino, Aventino, Campidoglio, Quirinale, Viminale, Esquilino na Celio.
Hali ya hewa
[hariri | hariri chanzo]Hali ya hewa hutawaliwa na bahari iliyo karibu. Wastani wa halijoto kwa mwaka ni sentigredi 15,4. Mvua hunyesha wastani wa mm 758 kwa mwaka.
Miezi yenye joto ni Juni hadi Agosti ikiwa na wastani wa sentigredi 21 hadi 23,8; ni miezi ya mvua kidogo.
Mwezi baridi zaidi ni Januari ikiwa na wastani wa sentigredi 7,9.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Historia ya mji inasemekana imeanza rasmi tarehe 21 Aprili 753 KK, lakini majengo ya kwanza ni ya karne ya 10 KK.
Katika karne za KK ulikuwa mji mkuu wa ufalme wa Roma, halafu wa Jamhuri ya Roma, hatimaye wa Dola la Roma.
Katika miaka 100 KK - 400 BK hivi ulikuwa na wakazi wengi kuliko miji yote duniani.
Uenezi wa Ukristo kuanzia mwaka 30 na hasa ujio wa Mtume Petro na Mtume Paulo waliofia dini yao (64-68) huko viliathiri mji huo moja kwa moja.
Kuanzia karne ya 7 BK ukawa mji mkuu wa Dola la Papa, halafu wa Ufalme wa Italia na sasa wa Jamhuri ya Italia. Huitwa mara nyingi "Mji wa Milele".
Wakazi
[hariri | hariri chanzo]Roma ilianza kama muungano wa vijiji vidogo vyenye wakazi mia kadhaa.
Katika karne ya 1 BK ilikuwa tayari na wakazi milioni moja.
Tangu kuondoka kwa makao makuu ya Kaisari na kupungua kwa nguvu ya Dola la Roma Magharibi idadi ya wakazi ilipungua hadi kuwa na takriban 100,000 mnamo mwaka 530.
Katika karne zilizofuata Italia pamoja na Ulaya iliona vita na mashambulio ya makabila yasiyostaarabika. Mnamo mwaka 1000 Roma ilikuwa mji mdogo wenye wakazi 20,000 pekee walioishi ndani ya maghofu ya mji mkubwa wa kale.
Tangu kuimarika kwa utawala wa mapapa mji ulianza kukua tena; mnamo mwaka 1900 ukawa na wakazi 400,000. Katika karne ya 20 mji ulipanuka sana hadi kufikia idadi ya wakazi wa zamani hata kuipita. Siku hizi asilimia 7.4 ni wageni.
Orodha inayofuata inaonyesha makadirio hadi 1858, baadaye ni namba za sensa.
|
|
Uchumi
[hariri | hariri chanzo]Roma ndiyo kitovu kimojawapo cha sekta ya viwanda na sekta ya huduma ya Italia. Utalii ni pia muhimu sana kiuchumi, kutokana na watalii 26,100,000 wanaoutembelea kila mwaka: 6.5% za Jumla ya Pato la Taifa zinapatikana ndani ya Roma ambazo ni kushinda miji mingine yote ya Italia.
Roma ina makao makuu ya F.A.O. (Food and Agriculture Organisation - Shirika la Chakula na Kilimo) ya Umoja wa Mataifa pamoja na ofisi zote za serikali ya Italia.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Sorrentino, Paolo (2014-12-17). "Da Comune a Capitale. Storia dell'identità visiva di Roma". Logos. 2 (24). doi:10.12957/logos.2014.14153. ISSN 1982-2391.
- ↑ Understanding China today : an exploration of politics, economics, society, and international relations. Silvio Beretta, Axel Berkofsky, Lihong Zhang. Cham, Switzerland. 2017. ISBN 978-3-319-29625-8. OCLC 990777946.
{{cite book}}
: CS1 maint: location missing publisher (link) CS1 maint: others (link) - ↑ Bahr, Ann Marie B. (2004). Christianity. Philadelphia: Chelsea House Publishers. ISBN 978-1-4381-0639-7. OCLC 613205976.
- ↑ D'Agostino, Peter R. (2004). Rome in America : transnational Catholic ideology from the Risorgimento to fascism. Chapel Hill: University of North Carolina Press. ISBN 0-8078-6341-6. OCLC 57707254.
- ↑ "What is the smallest country in the world?". History.com. Archived from the original on 27 September 2018. Retrieved 27 September 2018.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Rome travel guide kutoka Wikisafiri (Kiingereza)
- Info-Roma Ilihifadhiwa 23 Machi 2018 kwenye Wayback Machine. - Info-Rome ni tovuti kuhusu mambo ya kitalii katika mji wa Roma, hasa matukio ya aina mbalimbali, hoteli, maonyesho, nyumba za kumbukumbu na vyakula.
- (Kiingereza) some quick facts about Rome Ilihifadhiwa 15 Novemba 2005 kwenye Wayback Machine.
- (Kiingereza) Satellite image of Rome Ilihifadhiwa 28 Oktoba 2003 kwenye Wayback Machine. at NASA's Earth Observatory
- Rome Travel Guide Guide about Rome with touristic informations
- Rome map Ilihifadhiwa 14 Juni 2006 kwenye Wayback Machine. 360° IPIX PANORAMA
Makala hii kuhusu maeneo ya Italia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Roma kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |