Basilika la Mt. Petro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Basilika la Mt. Petro
Hii ni sehemu ya mfululizo kuhusu
Kanisa Katoliki
Imani

Umoja wa Mungu
Utatu (Baba, Mwana, Roho Mtakatifu)
Umwilisho Maisha ya Yesu
Msalaba Ufufuko Kupaa
Historia ya Wokovu Ufunuo
Biblia Mapokeo Ualimu Dogma
Neema Dhambi Wokovu Sakramenti
Watakatifu Bikira Maria

Muundo

Papa: Fransisko
Urika wa maaskofu Mitaguso mikuu
Kundi la Makardinali
Kanisa la Kilatini
Makanisa Katoliki ya Mashariki

Historia

Historia Ukristo
Ukatoliki Mlolongo wa Kitume
Sifa nne za Kanisa Utetezi Ekumeni
Maisha ya kiroho Amri Kumi Utawa
Sala Falsafa Teolojia
Muziki Sanaa Sayansi

Ibada

Liturujia Mwaka wa Kanisa
Ekaristi Liturujia ya Vipindi

Mapokeo ya liturujia

Liturujia ya Kilatini (Roma Liturujia ya Trento Milano Toledo Braga Lyon Canterbury)
Liturujia ya Armenia Liturujia ya Misri
Liturujia ya Ugiriki Liturujia ya Antiokia
Liturujia ya Mesopotamia

Basilika la Mt. Petro mjini Roma ni kanisa kubwa kuliko yote duniani na linatumiwa sana na Papa, ingawa si Kanisa kuu la jimbo lake.

Basilika hilo lote liko ndani ya eneo la Vatikani ambalo ni dola au nchi huru ndogo iliyoko ndani ya mji wa Roma (makao makuu ya Italia).

Kumbukumbu ya kutabarukiwa kwake inafanyika kila mwaka tarehe 18 Novemba[1].

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kanisa hili lilianzishwa mnamo mwaka 324 na Kaisari Konstantino Mkuu aliyeagizwa ujenzi mahali ambapo watu waliamini Mtume Petro aliuawa kwa ajili ya imani ya Ukristo akazikwa wakati wa Kaisari Nero (kabla ya mwaka 68).

Kanisa hilo la kale lilionekana bovu wakati wa karne ya 16, hivyo Papa Julius II aliamuru libomolewe ili kujenga kanisa jipya.

Muda wa ujenzi ulikuwa miaka 120: ulianza mwaka 1506 ukakamilishwa mwaka 1626.

Wasanii mashuhuri walishiriki katika ujenzi na upambaji wa kanisa hili kama vile Raphael, Michelangelo na Gian Lorenzo Bernini.

Ujenzi wake uligharamia pesa nyingi. Wataalamu wengi huona ujenzi huu ulikuwa sababu moja ya Matengenezo ya Kiprotestanti yaani farakano na Kanisa Katoliki lililoanzia Ujerumani katika karne ya 16.

Ni kwamba Mapapa walianzisha kodi mpya kwa waumini ili waweze kuendeleza ujenzi. Madai ya pesa kwa ajili ya ujenzi huo yaliendeshwa kwa ukali uliosababisha upinzani wa Martin Luther na wengine hasa huko Ujerumani.

Vipimo[hariri | hariri chanzo]

Kanisa hili lililojengwa juu ya eneo la mita za mraba 15,160 linaweza kupokea umati wa watu 60.000.

Lina urefu wa mita 211.5 na kimo cha mita 132.5.

Ukumbi wake una urefu wa mita 187 na upana wa 27.50. Ukumbi wa pili una urefu wa mita 138.

Jengo lina kuba moja kubwa na makuba manane ya kando.

Ndani ya kanisa kuna altare 45, nguzo 800, sanamu kubwa 390 za watu wa Biblia, Watakatifu na Mapapa.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Basilika la Mt. Petro nyuma ya Mto Tiber.
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
  1. Martyrologium Romanum