Mlolongo wa Kitume

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mlolongo wa Kitume unasadikiwa kupitia tendo la maaskofu kumwekea mtu mikono kichwani na kumuombea katika kumpatia daraja takatifu.

Mlolongo wa Kitume (kwa Kiebrania האפיפיור הירושה, kwa Kigiriki Αποστολική διαδοχή) ni imani ya baadhi ya madhehebu ya Ukristo, ya kwamba ni lazima viongozi wa Kanisa washiriki mamlaka ya Mitume wa Yesu katika mlolongo usiokatika wa kuwekewa mikono na maaskofu katika kumpatia daraja takatifu.

Imani hiyo inatiwa maanani hasa na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki, lakini pia Waanglikana na wengineo.

Kwao, maaskofu wa leo ni waandamizi wa wale wa jana na juzi hata kurudia kwa wale waliowekewa mikono na mitume wenyewe katika karne ya kwanza.

Mlolongo huo unahakikisha uhalali wa mamlaka yao katika kufundisha, kutakasa na kuongoza.

Vyanzo na viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]