Waanglikana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Altare ya St Mary Redcliffe, Bristol

Anglikana ni madhehebu ya Ukristo yenye asili ya Uingereza.

Katika karne ya 16 mfalme Henry VIII alitenga Kanisa la nchi hiyo na Kanisa Katoliki. Baada ya farakano hilo, yalifanyika mabadiliko mbalimbali upande wa imani, ibada na sheria kuelekea Uprotestanti. Hata hivyo mwelekeo wa Kikatoliki uliendelea kuwepo, na bado una nguvu, hasa katika baadhi ya dayosisi. Hasa miaka hii ya mwisho imeona mvutano kati ya pande hizo mbili kuongezeka hata kusababisha umoja kulegea.

Katika karne zilizofuata, kutokana na uenezi wa himaya ya Uingereza duniani, Anglikana ilienea sehemu nchi, na leo ina wafuasi wengi hasa Afrika (Nigeria, Uganda n.k.). Kwa jumla wanazidi milioni 70.

Majimbo yake 27 yanajitegemea,lakini yanaunda kwa pamoja ushirika mmoja. Maaskofu wake wote wanakutana Lambeth kila baada ya miaka 10 chini ya Askofu mkuu wa Canterbury.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]