Mitaguso ya kiekumene

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Mitaguso ya kiekumene (kutoka Kigiriki oικουμένη oikumene yaani dunia inayokaliwa na watu) ni jina la mikutano saba ya maaskofu ya kanisa la karne za kwanza wakati wa Mababu wa Kanisa iliyofanyika kati ya mwaka 325 hadi 787.

Mikutano hiyo ilitoa maamuzi ya kudumu juu ya mafundisho ya imani ya Kikristo yaliyokuwa muhimu kwa maendeleo ya Ukristo ya baadaye.

Yote ilitokea katika mashariki ya Dola la Roma iliyoendelea baadaye kama Milki ya Bizanti. ka Mitaguso hiyo saba inakubaliwa na Kanisa Katoliki, Kanisa la Kiorthodoksi, na pia katika madhehebu mengi ya Uprotestanti hasa Anglikana, Walutheri, Wamethodisti, Wamoravian na mengine.


1. Mtaguso wa kwanza wa Nikea (mwaka 325)

2. Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli (381)

3. Mtaguso wa Efeso (431)

4. Mtaguso wa Kalsedonia (451)

5. Mtaguso wa pili wa Konstantinopoli (553)

6. Mtaguso wa tatu wa Konstantinopoli (680-681)

7. Mtaguso wa pili wa Nikea (787)

Makanisa ya Waorthodoksi wa mashariki hukubali mitaguso mitatu ya kwanza tu. Madhehebu mengine ya kiprotestant yanakubali maazimio ya mitaguso kadiri jinsi yanavyolingana na uelewano wao wa Biblia.

Mitaguso ya kiekumene ya baadaye katika kanisa katoliki[hariri | hariri chanzo]

Kanisa katoliki limeendelea kuwa na mikutano ya maaskofu wake kutoka nchi zote za dunia likiendelea kuitazama kama mitaguso ya kiekumene.

Yafuatayo ni mitaguso inayohesabiwa katika kanisa katoliki:

8. Mtaguso wa nne wa Konstantinopoli (869-870)

9. Mtaguso wa kwanza wa Laterano (1123)

10. Mtaguso wa pili wa Laterano (1139)

11. Mtaguso wa tatu wa Laterano (1179)

12. Mtaguso wa nne wa Laterano (1215)

13. Mtaguso wa kwanza wa Lyon (1245)

14. Mtaguso wa pili wa Lyon (1274)

15. Mtaguso wa Vienne (1311-1312)

16. Mtaguso wa Kostansa (1414-1418)

17. Mtaguso wa Firenze (1439-1445)

18. Mtaguso wa tano wa Laterano (1512-1517)

19. Mtaguso wa Trento (1545-1563)

20. Mtaguso wa kwanza wa Vatikano (1869-1870)

21. Mtaguso wa pili wa Vatikano (1962-1965)


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]