Mtaguso wa tatu wa Laterano

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Basilika la Mtakatifu Yohane huko Laterano ambamo mtaguso ulifanyika.

Mtaguso wa tatu wa Laterano uliitishwa na Papa Aleksanda III (1159-1181) ufanyike huko Roma mwaka 1179, kutokana na Amani ya Venezia kati ya Kaisari Federiko I wa Ujerumani na Lega Lombarda ya Italia kaskazini.

Unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na moja.

Ulihudhuriwa na viongozi wa Kanisa 300 na kufanyika katika vikao vitatu, tarehe 5 Machi, 7 Machi na 19 Machi 1179.

Ulijadili masuala mbalimbali na kuyatungia kanuni 27 na kutangua zile zilizotolewa na antipapa Paskali III. Kati ya maamuzi muhimu zaidi, mmojawapo ulihusu uchaguzi wa Papa, ukidai thuluthi mbili za kura za makardinali wote, bila ya kutofautisha haki za makundi yao matatu.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtaguso wa tatu wa Laterano kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.