Mtaguso wa kwanza wa Vatikano
Sehemu ya mfululizo kuhusu |
Mitaguso mikuu ya Kanisa Katoliki |
---|
Mtangulizi (50 hivi) |
Roma ya Kale (325–451) |
Mwanzoni mwa Karne za Kati (553–870) |
Mwishoni mwa Karne za Kati (1122–1517) |
Nyakati za uvumbuzi mwingi (1545–) |
Mtaguso wa kwanza wa Vatikano unatazamwa na Kanisa Katoliki kama Mtaguso Mkuu wa ishirini katika historia yake.
Uliitishwa rasmi na Papa Pius IX (1846-1878) mnamo 29 Juni 1867 na vikao vyake viliendelea katika Basilika la Mt. Petro huko Vatikano mjini Roma kuanzia tarehe 8 Desemba 1869 hadi vilipokatika mnamo 1870 kutokana na jeshi la Italia kuteka Roma tarehe 20 Septemba.
Walishiriki maaskofu na mapadri 774 (kati ya 1050 wenye haki ya kuhudhuria), ambao kwa mara ya kwanza walitokea mabara yote. Pia ilikuwa mara ya kwanza ya kutokuwepo wawakilishi wa serikali. Kumbe wajumbe wa Waorthodoksi na wa Waprotestanti walialikwa pia, lakini hawakufika.
Tarehe 24 Aprili 1870, baada ya majadiliano mengi, ilipitishwa hati "Dei Filius" juu ya Mungu, ufunuo, imani, na uhusiano kati ya imani na akili.
Ingawa lengo halikuwa hilo, tokeo kuu la kazi ya mtaguso huo ni tangazo la dogma ya Papa kuwa na karama ya kutokosea katika mafundisho ya imani na maadili anayoyatoa ili yadumu moja kwa moja pale anapotimiza masharti fulani (kwa kifupi: akisema "ex cathedra", yaani "kutoka ukulu).
Dogma hiyo iliimarisha mamlaka ya Papa na umoja wa Kanisa dhidi ya maelekeo ya kitaifa ambayo yalitawala karne zilizotangulia yakisababisha matatizo mengi.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Hati za Mtaguso huo kwa Kiingereza. Archived 18 Agosti 2005 at the Wayback Machine.
- Kitabu THE TRUE AND THE FALSE INFALLIBILITY OF THE POPES Archived 27 Septemba 2006 at the Wayback Machine. *Kuhusu Askofu Joseph Fessler (1813-1872), katibu mkuu wa mtaguso.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mtaguso wa kwanza wa Vatikano kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |