Umoja
Mandhari
Umoja katika hisabati unahusu sifa maalumu za namba moja na za mambo yote yasiyo na wingi.
Kutokana na maana hiyo ya msingi, neno umoja linatumika katika fani mbalimbali, kuanzia dini, ambapo katika imani ya wengi (kama vile Wayahudi, Wakristo na Waislamu) umoja ni hasa sifa ya Mungu.
Katika Ukristo, imani katika umoja wa Mungu katika Nafsi tatu (Baba, Mwana na Roho Mtakatifu) ndio msingi wa umoja wa Kanisa pia kadiri ya Kanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli kwa njia ya ubatizo uleule mmoja ambao waamini wote wanatakiwa kuupokea.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |