Mungu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Alama ya Wasumeri iliyomaanisha dingir, mungu (mmojawapo).
Mabadiliko ya uandishi wa herufi nne za Kiebrania YHWH, jina maalumu la Mungu katika Biblia ya Kiebrania.
Jina la Allah, Mungu, kwa herufi za Kiarabu.

Mungu ni jina linalotumika kwa yeyote anayesadikiwa katika dini mbalimbali kuwa na uhai wa hali ya juu.

Kati ya wafuasi wa dini hizo, wengi wanaona kuwa Umungu, kwa jinsi ulivyo au unavyofirika, haukubali mgawanyiko. Hasa katika Uyahudi, Ukristo na Uislamu wanasisitiza umoja wa Mungu kuwa ndio msingi wa imani yao. Kwao Mungu ni wa milele, anafahamu yote na kutaka hasa uwepo wa viumbe. Tena kwa hiari yake alipenda kujifunua kwa binadamu; kielelezo ni Ibrahimu/Abrahamu aliyefanywa rafiki yake na baba wa waamini wote.

Kuna dini nyingine zinakubali kuwepo kwa miungu mbalimbali (wawili au zaidi). Hasa dini nyingi za jadi zinaamini uwingi wa miungu. Dini kubwa duniani inayosadiki miungu mingi ni Uhindu. Pia katika sehemu za Afrika ya Magharibi ibada za miungu mingi inaendelea hadi leo.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikiquote-logo.svg
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Icon-religion.png Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mungu kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.