Nenda kwa yaliyomo

Uhindu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uhindu
हिन्दू धर्म (Hindū Dharma)

ukubwa_wa_picha
Alama ya Om, ishara ya Uhindu

Uainishaji ya Kiasia (Dharmic)
Maandiko Veda
Upanishad
Bhagavad Gita
Mahabharata
Ramayana
Teolojia Mitazamo mbalimbali (Upweke, Upolotheistiki, Uungu Mmoja) [1]
Eneo Hasa Uhindi, Nepal, Bangladesh, na Diaspora ya Kihindu
Lugha Kisanskriti, na lugha za kienyeji za Uhindi
Mwaasisi Hakuna mwanzilishi maalum (dini ya kale). [2]
Asili Milenia ya 2 KK, Bonde la Indus
Ibada Sala, Yajna, Yoga, Homa, Pujā, Kusoma maandiko
Wafuasi Takriban bilioni 1.2

Uhindu (kwa Kisanskrit: हिन्दू धर्म: Hindū Dharma; pia सनातन धर्म Sanātana Dharma) ni dini kubwa yenye asili katika Bara Hindi.Ikiwa na wafuasi milioni 900 ni dini ya tatu baada ya Ukristo na Uislamu kwa wingi wa waumini.

Nchi zenye Wahindu

[hariri | hariri chanzo]

Katika nchi za India, Nepal na Morisi na kwenye kisiwa cha Bali (Indonesia) wakazi wengi hufuata aina mojawapo ya Uhindu.

Vikundi vikubwa viko pia:

Neno Hindu linatokana na lugha ya Kisanskrit ambapo Sindhu ni jina la kale la mto Indus uliopo kwenye sehemu ya magharibi kaskazini ya Bara Hindi. "Hindu" imepatikana mara ya kwanza wakati wa karne ya 6 KK katika andishi la mfalme Darius I kwa maana ya "watu wa ng'ambo ya mto Indus (Kisanskrit: Sindhu).[3] Hapa "Sindhu / Hindu" haina maana ya kidini bali ya kijiografia pekee.

Katika Kiajemi neno "Hindu" linamaanisha wakazi wa Uhindi pamoja na wafuasi wa dini kubwa ya nchi hiyo. Mnamo karne ya 11 milki iliundwa na Waajemi katika Bara Hindi iliyoitwa "Hindustan" na mji mkuu ulikuwa Lahore[4].

Baadaye Waingereza walipokea jina hilo kutoka Kiajemi, wakilitumia kwanza kwa nchi na baadaye hasa kwa wafuasi wa dini zisizo za Kiislamu, Kiyahudi wala Kikristo. Jina Hinduism (iliyoandikwa mwanzoni Hindooism) lilikuwa kawaida tangu karne ya 18 kwa kutaja falsafa na dini zenye asili ya India.[5]

  1. Pew research. "Theolojia ya Uhindu" (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-02-18.
  2. "origin of Hindu". Gettysburg.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-02-18.
  3. Flood, Gavin D. (1996), An Introduction to Hinduism, Cambridge University Press, uk. 6
  4. J. T. P. de Bruijn, makala HINDU kwa Encyclopædia Iranica Vol. XII, Fasc. 3, pp. 311-312, inapatikana online kwa http://www.iranicaonline.org/articles/hindu, ilitazamiwa 6-05-2016
  5. Will Sweetman (2003), Mapping Hinduism: 'Hinduism' and the Study of Indian Religions, 1600-1776, Otto Harrassowitz Verlag, ISBN 3-931479498, pages 163, 154-168

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.