Bara Hindi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Bara Hindi inavyoonekana kutoka angani

Bara Hindi ni eneo kubwa ya Asia upande wa kusini ya milima ya Himalaya lenye kilomita za mraba milioni 4.5. Inaingia ndani ya bahari Hindi kama rasi kubwa sana lenye umbo la pembetatu.

Nchi za Bara Hindi[hariri | hariri chanzo]

Nchi zifuatazo ni sehemu za Bara Hindi:

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Kijiografia kuna sehemu tatu za:

  • maeneo ya Himalaya (kaskazini ya Uhindi na Pakistan, Nepal, Bhutan)
  • rasi ya Uhindi
  • maeneo ya visiwa vya Bahari Hindi (Sri Lanka, Maldivi)

Kijiolojia Bara Hindi si sehemu ya Asia. Inakaa juu ya Bamba la Uhindi ambalo ni bamba la gandunia lililokuwa kama kisiwa kikubwa ndani ya Bahari Hindi hadi kujisukuma dhidi ya Bamba la Asia takriban miaka milioni 10 iliyopita. Mshtuko wa mgongano huu ulisababisha kukunja kwa ganda la dunia na kutokea kwa nyororo za milima ya Himalaya.