Kisiwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Visiwa)
Jump to navigation Jump to search
Picha:Island.jpg
Kisiwa kidogo
Kisiwa kidogo au mwamba tu?

Kisiwa ni eneo la nchi kavu ndani ya bahari, ziwa au mto linalozungukwa na maji wakati wote. Ukubwa wake hautoshi kuitwa "bara".

Visiwa vilivyoko karibu kama kundi mara nyingi huitwa "funguvisiwa".

Tofauti kati ya kisiwa kikubwa na bara dogo limeamuliwa kati ya

  • Greenland inayoitwa kisiwa kikubwa duniani chenye eneo la kilomita za mraba milioni 2.1 na
  • Australia inayotazamiwa kuwa bara dogo duniani lenye eneo la kilomita za mraba milioni 7.7.