Ziwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ziwa Tanganyika ni kati ya maziwa makubwa ya dunia (picha kutoka angani ya 1985
Ziwa katika Bariloche (Argentina)
Ziwa dogo milimani ya Ufaransa
Ufini inajulikana kama "Nchi ya Maziwa Maelfu".[1]

Ziwa ni gimba kubwa la maji linalozungukwa na nchi kavu pande zote. Tofauti na bahari ni ukubwa na kutobadilishana maji na bahari kuu. Lakini maziwa kadhaa yamepewa pia jina la "bahari" hasa kama yana maji ya chumvi au kama watu wa eneo lake hawajui magimba makubwa zaidi ya maji. Mfano wake ni Bahari Kaspi katika Asia ambayo ni kubwa sana lakini hali halisi ni ziwa lenye maji ya chumvi.

Mara nyingi mito inaingia au kutoka katika ziwa.

Maziwa mengi yana maji matamu kama maziwa makubwa ya Afrika ya Mashariki kwa mfano Viktoria Nyanza au Ziwa Nyasa au maziwa makubwa ya Amerika Kaskazini.

Lakini kuna pia maziwa yenye maji ya chumvi kama Bahari ya Chumvi kati ya Yordani na Israel au Bahari ya Kaspi kati ya Urusi na Uajemi.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Li, Leslie (1989-04-16). "A Land of a Thousand Lakes". The New York Times (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-12-29.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ziwa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.