Ufini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Suomen tasavalta
Republiken Finland

Jamhuri ya Ufini
Bendera ya Ufini Nembo ya Ufini
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: none
Wimbo wa taifa: Maamme (Kifini)
Vårt land (Kiswidi)
("Nchi yetu" Kiswahili)
Lokeshen ya Ufini
Mji mkuu Helsinki
60°10′ N 24°56′ E
Mji mkubwa nchini Helsinki
Lugha rasmi Kifini (89.33%), Kiswidi (5.34%)
Serikali Jamhuri2
Sauli Niinistö
Juha Sipilä
Uhuru
imetangazwa
6 Desemba 1917
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
338,145 km² (ya 64)
9.4
Idadi ya watu
 - 2014 kadirio
 - 2000 sensa
 - Msongamano wa watu
 
5,470,820 (ya 115)
5,181,115
16/km² (ya 201)
Fedha Euro (€)1 (EUR)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
EET (UTC+2)
EEST (UTC+3)
Intaneti TLD [.fi]
Kodi ya simu +358

-

1Prior to 1999: Finnish markka
2Semi-presidential systemUfini (pia: Finland, Finlendi; kwa Kifini: Suomi) ni nchi ya Skandinavia iliyoko Ulaya ya Kaskazini. Imepakana na Norwei upande wa kaskazini, Urusi upande wa mashariki na Uswidi upande wa magharibi.

Ng'ambo ya Baltiki iko Estonia ambayo watu wake hutumia lugha iliyo karibu sana na Kifini. Inaonekana ya kwamba mababu wa Wafini na Waestonia walihama pamoja wakiwa na lugha ileile zamani, lakini sasa ni lugha mbili kwa sababu hawakuwa na mawasiliano kati yao kwa muda mrefu.

Nchi ina wakazi milioni tano unusu tu katika eneo la km² 338,000; hivyo ni kati ya nchi za Ulaya zenye msongamano mdogo wa watu. Sehemu kubwa ya eneo lake ni misitu tu.

Mji mkuu ni Helsinki.

Nchi ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa na wa Umoja wa Ulaya.

Watu[hariri | hariri chanzo]

Kuna jumuiya tatu katika Ufini: Wafini wenyewe ambao ni 90% ya wakazi wote. Waswidi wako hasa upande wa kusini mwa nchi, kwa jumla ni takriban 5% ya wakazi. Hasa visiwa vya Aland kuna Waswidi watupu walio na hali ya kujitawala ndani ya Ufini. Wakazi asilia ni Wasami ambao wako kaskazini tu. Maisha yao yanategemea uwindaji na ufugaji; wako wachache, jumla yao haifikii 0.2% ya wakazi wote.

Mbali na hao, kuna wahamiaji (5.9%), hasa kutoka Russia, Estonia na Somalia.

Lugha rasmi ni Kifini na Kiswidi. Lugha ya Kifini ina asili ya Asia ya kati, haina uhusiano na lugha za Kihindi-Kiulaya.

Wakazi wenye lugha ya Kiswidi wako upande wa kusini mwa nchi kwa sababu Ufini ilitawaliwa na Uswidi kwa karne nyingi. Katika karne hizo walikuwepo Waswidi waliohamia Ufini lakini kuna pia Wafini walioanza kutumia Kiswidi pekee. Hasa kwenye visiwa vya Aland Kiswidi ni lugha pekee. Lakini Waswidi wa Ufini wanajisikia wa Ufini.

Upande wa dini, 73% ni Walutheri na 1.1% Waorthodoksi. Madhehebu hayo mawili ya Ukristo yanatambulika na kupewa nafasi katika matukio na shuleni. 24.3% hawana dini yoyote.

Watu maarufu[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]


Nchi za Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Denmark | Estonia | Hispania | Hungaria | Ireland | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituania | Luxemburg | Malta | Poland | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Ufalme wa Muungano | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Europa Mapa.png Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ufini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.