Luxemburg

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Groussherzogtum Lëtzebuerg
Grand-Duché de Luxembourg
Großherzogtum Luxemburg

Utemi mkubwa wa Luxemburg
Bendera ya Luxemburg [[Picha:|110px|Nembo ya Luxemburg]]
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Kiluxemburg: Mir wëlle bleiwe wat mir sinn
(Kiingereza: "Tunataka kukaa jinsi tulivyo")
Wimbo wa taifa: Ons Hémécht
("Nchi yetu")
WImbo wa kifalme: De Wilhelmus 1
Lokeshen ya Luxemburg
Mji mkuu Luxemburg
49°36′ N 6°7′ E
Mji mkubwa nchini Luxemburg
Lugha rasmi Kifaransa, Kijerumani, Kiluxemburg
Serikali
Mtemi mkubwa
Waziri Mkuu
Utemi Mkubwa
Mtemi Mkubwa Henri
Jean-Claude Juncker
Uhuru
Ilitangazwa
Ilithebitishwa
1815
1839
1867
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
2,586 km² (ya 176)
--
Idadi ya watu
 - 2014 kadirio
 - 2001 sensa
 - Msongamano wa watu
 
549 680 (ya 170)
439,539
194.1/km² (ya 60)
Fedha Euro ()2 (EUR)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
CET (UTC+1)
CEST (UTC+2)
Intaneti TLD .lu3
Kodi ya simu +352

-


Ramani ya Luxemburg

Luxemburg (pia: Lasembagi) ni nchi ndogo katika Ulaya. Imepakana na Ubelgiji, Ufaransa na Ujerumani.

Ikiwa na wakazi 550,000 kwenye eneo la km² 2,586 pekee ni nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya, tena ilikuwa kati ya nchi sita zilizoanzisha Jumuiya ya Kiuchumi ya Ulaya mwaka 1957.

Lugha ya wakazi wengi ni Kiluxemburg ambayo ni lahaja ya Kijerumani yenye athira nyingi za Kifaransa. Karibu watu wote huweza kuongea lugha hizo zote tatu.

Upande wa dini, 68.7% ni Wakatoliki na 3.7% ni Wakristo wa madhehebu mengine.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Luxemburg kama nchi ndogo ilikuwa mara nyingi chini ya athira ya majirani wakubwa waliotawala juu yake kwa vipindi mbalimbali.

Kwa vipindi vingi vya historia yake Luxemburg ilikuwa sehemu ya Ujerumani.

Katika karne ya 14 watemi wa Luxemburg walichaguliwa kuwa wafalme wa Ujerumani.

Baada ya vita za Napoleoni, Ufaransa na Prussia zilivutana juu ya Luxemburg. Walipatana kwenye Mkutano wa Vienna (1815) ya kurudisha Luxemburg kama nchi ya pekee itakayotawaliwa na Mtemi Mkubwa. Mfalme wa Uholanzi alikuwa mtemi wa Luxemburg na nchi yenyewe iliungwa katika Shirikisho la Ujerumani.

Baada ya mwisho wa Shirikisho la Ujerumani (1866) Luxemburg haikujiunga (1870) na Dola jipya la Ujerumani.

Badiliko la familia ya kifalme katika Uholanzi lilisababisha uchaguzi wa mtemi wa pekee.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Nchi za Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Denmark | Estonia | Hispania | Hungaria | Ireland | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituania | Luxemburg | Malta | Poland | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Ufalme wa Muungano | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Europa Mapa.png Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Luxemburg kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.