Kijerumani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hadhi ya Kijerumani katika nchi mbalimbali.
Hadhi ya Kijerumani katika nchi mbalimbali.
Nchi ambako lugha ya Kijerumani huzungumzwa.

Kijerumani (pia: Kidachi, kwa Kijerumani: Deutsch au (die) deutsche Sprache) ni lugha ya Kigermanik ya magharibi katika jamii ya lugha za Kihindi-Kiulaya.

Huzungumzwa hasa katika nchi za Ujerumani, Austria, Uswisi, Liechtenstein na Luxemburg.

Kuna pia wasemaji asilia katika nchi jirani za Ujerumani / Austria kama Ubelgiji, Uholanzi, Ufaransa, Denmark, Poland na Italia ya kaskazini. Nchi nyingi za Ulaya ya Mashariki zilikuwa na wasemaji wa Kijerumani lakini wengi walifukuzwa au kuondoka wakati wa vita kuu ya pili ya dunia; vikundi vimebaki hasa katika Hungaria, Romania, Uceki, Urusi na Kazakhstan.

Vikundi vidogo vya watu waliohamia katika karne za 19 na 20 wanaoendelea kutumia Kijerumani wako katika Amerika ya Kaskazini (Marekani, Kanada), Amerika Kusini (Brazil, Chile) na Afrika (hasa Namibia na Afrika Kusini).

Kijerumani huzungumzwa na watu milioni 100 katika Ulaya. Ni lugha ya pili katika Ulaya baada ya Kirusi kushinda Kifaransa na Kiingereza.

Kijerumani kama lugha ya kitaifa[hariri | hariri chanzo]

Kijerumani kinatumiwa kama lugha rasmi kitaifa katika nchi zifuatazo:

Lugha rasmi kieneo[hariri | hariri chanzo]

Kijerumani kinatumiwa kama lugha rasmi ya utawala kieneo (ama kimkoa au kwenye ngazi ya miji / tarafa tu) katika nchi zifuatazo:

Umoja wa Ulaya[hariri | hariri chanzo]

Kijerumani ni kati ya lugha rasmi za Umoja wa Ulaya pamoja na Kiingereza na Kifaransa. Kati ya lugha ndani ya Umoja ni lugha yenye wasemaji wengi kushinda nyingine zote.

Maneno machache[hariri | hariri chanzo]

hujambo? – sijambo Wie geht es dir? – Mir geht es gut.
jambo Hallo!
ndiyo ja
hapana nein
mgeni Gast, Fremder
rafiki Freund
karibu Willkommen!
kwa heri Auf Wiedersehen!
asante Danke!
asante sana Vielen Dank!
safari Reise
ninakupenda Ich liebe dich.
hatari Gefahr
daktari Doktor
polepole langsam
Afya! (wakati wa kunywa na mwingine) Prost!
kijiji Dorf
mji Stadt

Lugha inayofundishwa[hariri | hariri chanzo]

Kijerumani kama lugha ya kigeni kinafundishwa shuleni au kwenye taasisi za elimu ya watu wazima katika nchi nyingi. Mwaka 2004 idadi ya wanafunzi wa Kijerumani ilikuwa kama ifuatayo:

Kijerumani ni lugha ya pili katika mtandao (intaneti) baada ya Kiingereza. Takriban nusu ya kurasa zote mtandaoni ni za Kiingereza, lakini Kijerumani kinafuata kikiwa na 8% za kurasa zote.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]