Lugha za Kihindi-Kiulaya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Usambazaji wa lugha za Kihindi-Kiulaya (kijani cheupe) kati ya jamii za lugha zingine duniani
Uenezaji wa wasemaji wa Kihindi-Kiulaya asilia kufuatana na nadharia ya Kurgan
Uenezaji katikati ya milenia ya 3 KK
Uenezaji katikati ya milenia ya 2 KK
Uenezaji takriban mwaka 250 KK

Lugha za Kihindi-Kiulaya ni jamii kubwa zaidi ya lugha zote duniani. Kuna wasemaji bilioni 2.5 katika mabara yote.

Uenezi huo umetokana hasa na historia ya ukoloni wa Kizungu uliopeleka lugha za Ulaya pande zote za dunia.

Lugha za Kihindi-Kiulaya

Jina la Kihindi-Kiulaya[hariri | hariri chanzo]

Jina la Kihindi-Kiulaya limepatikana tangu karne ya 19. Wataalamu walitambua ya kwamba lugha za kale zinazotunzwa kimaandishi kama Kilatini, Kigiriki, Kisanskrit na Kiajemi cha Kale zinafanana kati yake pia na lugha zingine za kisasa za Ulaya na Uhindi wa Kaskazini.

Lugha za jamii ya Kihindi-Kiulaya zinafanana katika msamiati na sarufi.

Nadharia ya asili na usambazaji[hariri | hariri chanzo]

Inaaminika ya kwamba lugha hizi zilikuwa na asili ya pamoja katika lugha isiyojulikana tena ya Kihindi-Kiulaya asilia.

Wasemaji wake wanaaminiwa kuwa walisambaa takriban miaka 6.000 iliyopita kutoka sehemu za Asia ya Magharibi. Sehemu ilihamia kwenda magharibi na kuingia Ulaya, sehemu nyingine ilihamia kwenda Uajemi na Bara Hindi.

Kuna nadharia mbalimbali kuhusu historia hiyo.

Kati ya lugha hizi kuna zifuatazo:

( † inamaanisha ya kwamba lugha hii haina wasemaji tena kama lugha hai)
Globe of letters.svg Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lugha za Kihindi-Kiulaya kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.