Lugha za Kiselti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani inayonyesha lugha hizo zinapotumika hadi leo au zilipotumika katika karne za mwisho:      Ireland (Kieire)      Scotland (Kiskoti)      Isle of Man (Kimanksi)      Wales (Kiwelisi)      Cornwall (Kikornishi)      Brittany (Kibretoni)

Lugha za Kiselti ni tawi la lugha za Kihindi-Kiulaya ambalo limerudi nyuma sana tangu zamani za Roma ya Kale lilipokuwa linatumika katika eneo kubwa sana la Ulaya hadi Uturuki wa leo.

Kati ya hizo, sita ni hai na ni lugha mama za watu 1,400,000 hivi[1].

Kati yake, Kieire ni lugha ya pili ya watu 1,865,000 hivi, hasa katika kisiwa cha Ireland na kwa sababu hiyo ni lugha ya taifa na lugha rasmi ya kwanza ya Eire. Kwa sababu hiyohiyo ni pia lugha rasmi mojawapo ya Umoja wa Ulaya.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Crystal, David (2010). The Cambridge Encyclopedia of Language. Cambridge University Press. ISBN 978-0-521-73650-3.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lugha za Kiselti kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.