Nenda kwa yaliyomo

Lugha ya kwanza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Lugha mama)
Mnara kwa lugha mama (ana dili) huko Nakhchivan, Azerbaijan.
Sikukuu ya lugha mama mjini Sydney, Australia, 19 Februari 2006

Lugha ya kwanza ni lugha ambayo mtu anaiongea kama lugha yake ya kwanza tangu utotoni[1], umri ambamo ni rahisi zaidi kuathiriwa na mazingira na hivyo pia kujifunza kusema kama watu wa kandokando [2] .

Pia lugha hiyo huitwa lugha mama (kwa Kiingereza "mother tongue") kwa vile watu wengi hujifunza lugha yao ya kwanza kutoka kwa mama mzazi. Lakini hiyo si lazima: mara nyingine mtoto halelewi na mama, au kama analelewa, anatumia muda mrefu zaidi na watoto wenzake (hasa shuleni), hivyo anazoea lugha yao kuliko ile ya nyumbani, hata kama ni tofauti kabisa.

Kwa sababu hiyohiyo wapo watu wenye lugha mama zaidi ya moja[3].

Tarehe 17 Novemba 1999, UNESCO iliteua tarehe 21 Februari ya kila mwaka kuwa Siku ya Kimataifa ya Lughamama.

  1. Bloomfield, Leonard. Language Archived 17 Januari 2023 at the Wayback Machine ISBN 81-208-1196-8
  2. "Terri Hirst: The Importance of Maintaining a Childs First Language". bisnet.or.id. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 13 Julai 2010.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Davies, Alan (2003). The Native Speaker: Myth and Reality. Multilingual Matters. ISBN 1-85359-622-1. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Januari 2023. Iliwekwa mnamo 20 Juni 2015.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lugha ya kwanza kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.