Mazingira

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mazingira ya kiafrika

Mazingira ni jumla ya mambo yote yanayomzuguka kiumbe katika maisha yake. Kwa hiyo kila unachokiona ni mazingira yako.

Mazingira huweza kuundwa na vitu mbalimbali; yanaweza kuwa ya asili (kama misitu, milima, maziwa, mabonde, mito, bahari n.k.) au ya kutengenezwa na binadamu (kama majengo, viwanda n.k.).

Hivyo tunapaswa tuwe makini katika kujenga mazingira yetu kwa sababu vitu vingine huyaharibu, kama vile uchafuzi wa hewa, uchafuzi wa bahari, uchafuzi wa ardhi, n.k.

Tunapaswa kutunza mazingira yetu kwa sababu kilimo, ufugaji mvua, n.k. huathiriwa na uchafuzi wa mazingira. Mazingira hutunzwa kwa njia mbalimbali kama vile kupanda miti kwa wingi, kutunza vyanzo vyetu vya maji, na kutumia maji vizuri, hasa katika shughuli za kilimo, ili kuliepuka tatizo la ukame.

Kanuni kuhusu ulinzi wa mazingira[hariri | hariri chanzo]

Nchi mbalimbali zina kanuni za ulinzi wa mazingira. Kwa mfano katika nchi ya Marekani, kuna kanuni kuhusu ulinzi wa wanyama wanaokaribia kutoweka. Kanuni hii iko katika sheria ya Endangered Species Act (ESA) iliyopitishwa na rais Richard Nixon mwaka 1973. Pia kuna mkataba wa kimataifa uitwao Convention on International Trade in Endangered Species of Wild Flora and Fauna (CITES). Barani Afrika, ulinzi wa mazingira waendeshwa pia japo kuna majangili wanapenda sana kukiuka sheria ili wajitajirishe kwa kuwinda wanyama kiharamu.

Kurasa kuhusu neno mazingira[hariri | hariri chanzo]

Mazingira yanaweza kuhusu:

  • Hifadhi ya mazingira
  • Uharibifu wa mazingira, vitu vinavyoweza kuchafua mazingira kama vile viwanda, wanyama n.k.
  • Kujenga mazingira, ujenzi wa eneo ili kuwezesha shughuli za binadamu
  • Biofizikia ya mazingira, pamoja na mwingiliano wa kemikali zinayoathiri viumbe hai
  • Mifumo ya mazingira, maeneo ya mfumo wa kimwili ambayo yanaweza kuingiliana na mfumo wa mazingira na kubadilishana molekuli, nishati n.k.
  • Sanaa ya mazingira
  • Mazingira pandikizi
  • Sera ya mazingira
  • Saikolojia ya mazingira
  • Ubora wa mazingira
  • Sayansi ya mazingira, utafiti wa mwingiliano kati ya hali ya kimwili, kemikali na majumuisho ya vitu vinavyohusu mazingira ya biolojia
  • Mfululizo wa mazingira, LPs, kaseti na CD zinazotoa milio ya asili
  • Maarifa ya mazingira
  • Mazingira ya asili, viumbe hai na visivyo hai ambavyo vimetokea kiasili duniani
  • Mazingira ya kijamii, tamaduni ambazo mtu hufuata
  • Ekolojia, ubora wa kibiolojia mara kwa mara huchanganywa katika mtazamo wa mazingira kwa ujumla
  • Harakati za mazingira
  • Uboreshaji wa mazingira
  • Orodha ya masuala ya mazingira
  • Mazingira ya Yesu

Katika sayansi ya kompyuta:

  • Mazingira ya mezani, graphical user interface kwa kompyuta
  • Mazingira yanayobadilikabadilika, sera ya kutambulisha mchakato wa kimazingira
  • Mwingiliano wa maendeleo ya mazingira, aina ya programu za kompyuta ya kusaidia katika kuendeleza wataalamu wa kompyuta ili kutengeneza programu
  • Mazingira ya wakati, hali ya mashine isiyo halisi ambayo inatoa huduma ya kuprogramu michakato au mipango ya kuprogramu wakati kompyuta ikiendelea kufanya kazi

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Simple English Wiktionary
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno: