Nenda kwa yaliyomo

Ujangili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Jangili)
Makumbusho ya vifaru waliouawa na majangili huko St Lucia Estuary, Afrika Kusini.

Ujangili au uwindaji haramu ni tendo la kuwinda wanyama bila kibali au kinyume cha sheria za nchi.

Kwa milenia nyingi kabla ya kubuniwa kwa kilimo na ufugaji, uwindaji ulikuwa njia ya kawaida kwa watu kujipatia chakula cha nyama.

Tangu kutokea kwa madola au mifumo mingine ya utawala wanyama wa windo walianza kuwa haba katika maeneo kadhaa na hapo watawala walilenga kutunza haki ya kuwinda kwao wenyewe tu. Hii ilikuwa hali ya kawaida katika Ulaya wakati wa karne za kati.

Mtazamo huo ulipelekwa Afrika wakati wa ukoloni. Pamoja na hayo, uwindaji ulionekana kuwa hatari kwa spishi za wanyama wenye thamani ya kibiashara, kama vile tembo waliowindwa kwa kulenga ndovu zao. Hata kabla ya ukoloni, tembo walikuwa walipungua tayari katika sehemu za Afrika ya Mashariki zilizo karibu na pwani.

Baada ya uhuru nchi nyingi zililenga kuweka taratibu za uwindaji zilizobana haki za wananchi kuwinda.

Pengine watu maskini wanakimbilia ujangili ili kupata mahitaji yao, lakini mara nyingi zaidi ni waroho ambao wanatafuta faida kubwa inayopatikana kwa njia hiyo, kwa mfano kwa kuua tembo na vifaru ili kunyofoa na hatimaye kuuza pembe zao.

Kama mtu anaiba mifugo ya wengine, si ujangili, bali wizi tu.

Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ujangili kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.