Uwindaji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mwindaji maarufu alivyochorwa na Diego Velázquez akiwa na silaha na mbwa.

Uwindaji (kwa Kiingereza Hunting) ni desturi ya kuua au kukamata wanyama, hasa kwa ajili ya kujipatia chakula, lakini pengine kwa biashara, burudani tu, kama si kwa kukomesha wanyama waharibifu.

Mbali ya uwindaji halali, kuna ujangili unaohatarisha aina mbalimbali za wanyama kiasi cha kuwamaliza kabisa duniani.

Kama mnyama husika ni samaki, kazi hiyo inaitwa uvuvi.

Kabla ya kuanza uzalishaji, kwa karne nyingi binadamu wote walitegemea hasa uchumaji wa matunda na uwindaji.