Ujangili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Makumbusho ya vifaru waliouawa na majangili huko St Lucia Estuary, Afrika Kusini.

Ujangili (kwa Kiingereza poaching) ni uwindaji haramu wa wanyama pori.

Pengine watu maskini wanakimbilia ujangili ili kupata mahitaji yao, lakini mara nyingi zaidi ni waroho ambao wanatafuta faida kubwa inayopatikana kwa njia hiyo, kwa mfano kwa kuua tembo na vifaru ili kunyofoa na hatimaye kuuza pembe zao.

Kama mtu anaiba mifugo ya wengine, si ujangili, bali wizi tu.