Kilimo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Kilimo ni uzalishaji wa mazao kwenye mashamaba. Kilimo kina maana pana inayojumuisha mifumo ya uzalishaji mimea, ufugaji wa wanyama, na uvuvi wa samaki. Mara nyingi kilimo cha mimea kinaenda sambamba na ufugaji wa wanyama.

Watu hupanda mimea na kuitunza hadi mavuno hasa kwa uzalishaji wa chakula cha kibindadamu na lishe ya wanyama lakini pia kwa shabaha ya kupata malighafi mbalimbali zinazotumiwa kwa kutengeneza nguo za watu. Siku hizi kilimo kinalenga pia nishati ya mimea.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Watu walianza kulima takriban miaka 10,000 iliyopita na kabla ya hayo watu walivinda tu na kukusanya matunda. Kuna vikundi vidogo ambavyo vinaendelea na maisha haya hadi leo lakini siku hizi zaidi ya asilimia 99 ya binadamu hupata chakula kutokana na kilimo.

Inaaminiwa ya kwamba kilimo kilianza katika sehemu tatu za dunia ambako watu walitambua mimea yenye lishe kubwa na kupanda mbegu zao. Maeneo haya ambako kilimo kilianza ni China, Amerika ya Kaskazini na Mashariki ya Kati. Wataalamu hawakubaliani kama kilimo cha Afrika kina asili yake huko Mashariki ya Kati au kama ilianzishwa barani peke yake.

ThreeCoins.svg Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kilimo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.