Mashariki ya Kati

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mashariki ya Kati pamoja na Uturuki.

Mashariki ya Kati ni namna ya kutaja sehemu kubwa ya Asia ya Magharibi pamoja na Afrika ya kaskazini-mashariki, hasa Misri.

Kwa kawaida nchi zifuatazo huhesabiwa humo:

Nchi hizi zinatajwa pamoja kwa sababu zina historia ya pamoja na utamaduni ni wa karibu kati yao.

Matatizo ya jina hili[hariri | hariri chanzo]

Jina "Mashariki ya Kati" limesambazwa kutokana na kawaida ya Kiingereza na kutafsiriwa katika lugha mbalimbali. Lina matatizo kadhaa yanayotakiwa kujulikana hata tukiendelea kulitumia:

  • kuna namna mbalimbali za kutaja nchi za zaida zinazohesabiwa humo au la (kwa mfano: wengine huhesabu pia nchi za Asia ya Kati kama vile Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan n.k.)
  • jina ni tamko la Kiulaya: nchi hizi ziko upande wa mashariki kwa mtu aliyeko Ulaya. Kutoka Uswahilini ingekuwa zaidi "Kaskazini ya Kati"
  • matumizi ya jina yamebadilika: zamani Kiingereza kilitofautisha kati ya
    • "Mashariki ya Karibu" (Near East),
    • "Mashariki ya Kati" (Middle East) na
    • "Mashariki ya Mbali" (Far East)

kikimaanisha

Lugha mbalimbali za Ulaya Bara kama Kijerumani zinaendelea kutumia majina haya matatu vile. Pia wataalamu wa historia kwa Kiingereza hupendelea kutofautisha kati ya "Mashariki ya Karibu" na "Mashariki ya Kati".

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]


Sciences de la terre.svg Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mashariki ya Kati kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.