Nenda kwa yaliyomo

Japani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Japani
日本国 Nihon-koku au Nippon-koku (Kijapani)
Wimbo wa taifa: 君が代
Kimigayo ("Utawala wa Mtukufu wa Kifalme")
Mahali pa Japani
Mji mkuu
na mkubwa
Tokyo
Lugha rasmiKijapani
Lugha ya taifaAinu (inayotambuliwa), Kiryukyuan, Hachijō (hazijatambuliwa)
 • Mfalme
Naruhito
 • Waziri Mkuu
Shigeru Ishiba
Historia
 • Katiba ya Meiji
29 Novemba 1890
 • Katiba ya sasa
3 Mei 1947
Eneo
 • Jumlakm2 377,975 (ya 62)
 • Maji (asilimia)1.4%
Idadi ya watu
 • Kadirio la 2025123,400,000
 • Msongamano330/km2
PLT (PPP)Kadirio la 2025
 • Jumla $6.741 trilioni
 • Kwa kila mtu $54,678
PLT (Kawaida)Kadirio la 2025
 • Jumladecrease $4.186 trilioni (ya 5)
 • Kwa kila mtudecrease $33,956
HDI (2023) 0.925 juu
Gini (2018)33.4
SarafuYen ya Kijapani (¥)
Majira ya saaUTCUTC+09:00 (JST)
Upande wa magariKushoto
Msimbo wa simu+81
Jina la kikoa.jp

Japani, ni nchi ya visiwa katika Asia ya Mashariki, iliyoko kwenye Bahari ya Pasifiki. Inapakana kwa maji na China, Korea Kusini, Korea Kaskazini, na Urusi. Ina idadi ya watu takriban milioni 123, ikiwa ya 11 duniani. Jiji lake kubwa zaidi na mji mkuu ni Tokyo, moja ya miji yenye watu wengi zaidi duniani. Japani imegawanyika katika mikoa 47, Inajulikana kwa teknolojia yake ya hali ya juu, utamaduni wake wa kale na wa kisasa kama anime na samurai, pamoja na miundombinu ya kisasa kama treni za mwendo kasi (Shinkansen).

Japani ni mojawapo ya nchi zilizoendelea zaidi kiuchumi duniani, ikiwa na mojawapo ya pato la taifa kubwa zaidi kwa viwango vya kimataifa. Uchumi wake unaegemea hasa katika viwanda vya teknolojia ya hali ya juu, magari, vifaa vya kielektroniki, na roboti. Makampuni makubwa kama Toyota, Sony, na Panasonic yanatoka Japani na yana ushawishi mkubwa duniani. Licha ya rasilimali chache za asili, Japani imefanikiwa kukuza uchumi wake kupitia ubunifu, elimu ya juu, na nidhamu ya kazi miongoni mwa wananchi wake.

Katika historia, Japani iliwahi kuwa milki ya kifalme iliyojitenga na mataifa ya nje kwa karne nyingi, hadi ilipofunguka kwa dunia wakati wa kipindi cha Meiji mnamo karne ya 19. Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, ambapo ilishambuliwa vikali ikiwemo mabomu ya atomiki mjini Hiroshima na Nagasaki, Japani ilijengwa upya na kuwa taifa la kidemokrasia. Leo, ni mwanachama wa mashirika makubwa kama Umoja wa Mataifa, G7, na G20, na ina ushawishi mkubwa katika siasa, uchumi, na utamaduni wa kimataifa.

Jiografia

Japani ni funguvisiwa lenye visiwa 14,125 mbele ya pwani ya Uchina, Korea na Urusi (Siberia).

Visiwa vikubwa na muhimu zaidi ni vinne tu; ndivyo Honshu, Hokkaido, Shikoku na Kyushu. Safu ya milima inapita visiwa vyote vikubwa na kusababisha msongamano mkubwa wa wakazi katika miji kutokana na uhaba wa ardhi ya kukalia. Hali halisi Japani yote ni safu ya milima tu inayopanda juu kutoka sakafu ya bahari na vilele vya milima yake huonekana juu ya uso wa bahari kama visiwa vikubwa au vidogo.

Kijiolojia eneo hili liko kwenye mstari ambako mabamba ya gandunia ya Ulaya-Asia, Pasifiki na Ufilipino hukutana. Hii ni sababu ya kuwepo kwa volkeno 240 katika Japani na takriban 40 kati ya hizo ni hai pia kutokea kwa matetemeko ya ardhi ya mara kwa mara. Hivyo Japani ni sehemu ya pete ya moto ya Pasifiki inayozunguka bamba la Pasifiki.

Japani inapatwa kila mwaka na dhoruba kali aina ya taifuni. Hata tsunami (ni neno la Kijapani) ni kawaida. Nchi inajikinga na mitambo mengi ya kutoa taarifa ya tsunami kuanza pia mitambo ya kufunga milango ya mabandari.

Nyumba ya kimapokeo.

Miji

Makala kuu: Miji ya Japan

Wajapani wengi hukalia sehemu ndogo ya 10% za nchi. Kuna miji kumi yenye wakazi zaidi ya milioni moja. Miji mikubwa ni Tokyo, Yokohama, Nagoya, Osaka, Kyoto, Kobe, Hiroshima, Fukuoka, Kitakyushu, Sendai na Sapporo. Usafiri ndani ya Japani ni hasa kwa treni, mabasi na ndege. Treni ya Shinkansen visiwani Honshu na Kyushu ni kati ya treni zenye mkasi mkubwa duniani.

Mikoa

Makala kuu: Mikoa ya Japani
Map of the prefectures of Japan in ISO 3166-2:JP order and the regions of Japan

Japan ina mikoa arubaini na saba. Kila mkoa unasimamiwa na gavana mmoja, bunge na urasimu utawala. Kila mkoa umegawanyika katika miji na vijiji.


1. Hokkaidō


2. Aomori
3. Iwate
4. Miyagi
5. Akita
6. Yamagata
7. Fukushima


8. Ibaraki
9. Tochigi
10. Gunma
11. Saitama
12. Chiba
13. Tokyo
14. Kanagawa


15. Niigata
16. Toyama
17. Ishikawa
18. Fukui
19. Yamanashi
20. Nagano
21. Gifu
22. Shizuoka
23. Aichi


24. Mie
25. Shiga
26. Kyoto
27. Osaka
28. Hyōgo
29. Nara
30. Wakayama


31. Tottori
32. Shimane
33. Okayama
34. Hiroshima
35. Yamaguchi


36. Tokushima
37. Kagawa
38. Ehime
39. Kōchi


40. Fukuoka
41. Saga
42. Nagasaki
43. Kumamoto
44. Ōita
45. Miyazaki
46. Kagoshima
47. Okinawa

Kwa sasa manispaa za Japani zinaundwa upya kwa kuunganisha mikoa, miji na baadhi ya vijiji. Mabadiliko hayo yatapunguza idadi ya miji nchini Japani.[1]

Historia

Visiwa vilikaliwa na binadamu tangu miaka 30,000 KK.

Wakazi wa sasa wametokana na mchanganyiko wa makabila asili (kama Waainu) na Wakorea waliovamia visiwa hivyo.

Uchumi

Japani ni nchi ya tatu duniani kwa ukubwa wa uchumi.

Dini

Wajapani wanaweza kushiriki ibada za dini mbalimbali kadiri wanavyojisikia, lakini asilimia 60 hawana dini maalumu. Wabuddha ni asilimia 34, wafuasi wa madhehebu ya Shinto ni asilimia 4, Wakristo sanasana ni asilimia 2.3.

Tazama pia

Tanbihi

  1. Mabuchi, Masaru (2001). "Municipal Amalgamation in Japan (PDF)" (PDF). World Bank. Iliwekwa mnamo 2006-12-28. {{cite web}}: Unknown parameter |month= ignored (help)

Marejeo

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
Utalii
Taarifa za jumla
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Makala hii kuhusu maeneo ya Japani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Japani kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.