Nenda kwa yaliyomo

Qatar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Katar)
دولة قطر
Dawlat Qatar

State of Qatar
Bendera ya Qatar Nembo ya Qatar
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa:
Wimbo wa taifa: As Salam al Amiri
Lokeshen ya Qatar
Mji mkuu Doha
25°18′ N 51°31′ E
Mji mkubwa nchini Doha
Lugha rasmi Kiarabu, Kiingereza
Serikali Ufalme
Tamim bin Hamad Al Thani
(تميم بن حمد بن خليفة آل ثاني)
Khalid bin Khalifa bin Abdul Aziz Al Thani
(خالد بن خليفة بن عبد العزيز آل الثاني)
Uhuru1
 
3 Septemba 1971
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
11,581 km² (ya 158)
„kidogo sana“
Idadi ya watu
 - Agosti 2020 kadirio
 - 2010 sensa
 - Msongamano wa watu
 
2,795,484 (ya 142)
1,699,435 [1]
176/km² (ya 76)
Fedha Riyal (QAR)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+3)
(UTC+3)
Intaneti TLD .qa
Kodi ya simu +974
1 Qatar ilitawaliwa na familia ya Al Thani tangu karne ya 19 lakini ilikuwa chini ya Uingereza katika karne ya 20


Qatar (kwa Kiarabu: قطر ) ni emirati ndogo wa Uarabuni kwenye rasi ya Qatar ambayo ni sehemu ya rasi kubwa ya Uarabuni.

Imepakana na Saudia upande wa kusini. Mipaka mingine ni ya Ghuba ya Uajemi. Kisiwa cha Bahrain kiko karibu.

Mji mkuu wa Qatar ni Doha.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Maeneo ya Qatar, pamoja na Falme za Kiarabu na Bahrain yalikuwa nyumbani kwa makabila madogo na chifu zao.

Tangu mwaka 1820 walikuwa na mikataba na Uingereza walipoahidi kuachana na uharamia na kupokea ulinzi wa Uingereza. Ulinzi huo ulizuia uvamizi wa Saudia katika karne ya 20.

Falme hizo zilikuwa nchi lindwa chini ya Uingereza hadi mwaka 1971, ambapo madola hayo madogo yalipata uhuru.

Miaka ya mwisho Qatar imejihusisha na siasa ya Mashariki ya Kati kwa kuwapa silaha Waislamu wenye itikadi kali kama vile huko Palestina, Syria na Iraq, na hata DAISH.

Kwa sababu hiyo imetengwa na nchi jirani, hasa Saudia.

Wananchi wengi wa Qatar kwa asili ni Waarabu na Waafrika (utumwa nchini ulichelewa sana kufutwa). Lakini kati ya wakazi wote, wenyeji hao ni asilimia 12 tu (313,000), yaani idadi kubwa sana si Waqatari wenyewe bali ni wafanyakazi kutoka nchi mbalimbali, hasa India (zaidi ya 21%) na nchi za kandokando yake (Nepal 16.6%, Bangladesh 12.5%, Pakistan 4.5%, Sri Lanka 4.3%), halafu Ufilipino (10%), Misri (9%) n.k.

Kiarabu ni lugha rasmi ya nchi lakini Kiingereza hutumiwa mara nyingi kwa mawasiliano ya biashara na ofisini.

Waqatari wenyewe ni Waislamu (hasa Wasuni) lakini watu kutoka nje hufuata pia dini mbalimbali: hivyo kati ya wakazi wote 65.5% ni Waislamu, 15.1% ni Wahindu, 14.2% ni Wakristo, 3.3% ni Wabuddha n.k.

Uchumi wote wa Qatar una msingi wa mafuta ya petroli na gesi yake. Kwa wastani wakazi wake wana kipato kikubwa kuliko watu wa nchi zote duniani.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Qatar kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.