Sana'a

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sana'a - صنعاء
Habari za kimsingi
Mkoa Mkoa wa Sana'a
Anwani ya kijiografia Latitudo: 15°21'N - Longitudo: 44°12'E
Kimo 2,200 m juu ya UB
Eneo ?? km²
Wakazi takriban milioni 2
Msongamano wa watu watu ?? kwa km²
Simu +967 (nchi), 1 (mji)
Mahali

Sana'a (Kiarabu: صنعاء) ni mji mkuu wa Yemeni mwenye wakazi 1,747,627 (2004). Iko kwa 15°21'N na 44°12'E kwenye nyanda za juu za Yemen kwenye kimo cha 2,200 m juu ya UB.

Mji uko takriban 300 km kaskazini ya Aden ambayo ni mji mkubwa wa nchi.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Sana'a imejulikana kama mji tangu karne ya 1 BK. Wataalamu huamini ya kwamba makazi ya kale zaidi yalitangulia hapa. Kuna hadithi ya kieneyeji inayodai kwamba mji uliundwa na Sem mwana wa Nuhu.

Ilikuwa mji mkuu wa milki ya Himyari hadi mwaka 520. Vita ya wenyewekwa wenyewe chini ya mfalme Yūsuf Asar Dhū Nuwas ilisababisha kuingilia kati kwa Wahabeshi wa Aksum walioteka mji. Wakati ule kanisa kubwa kusini ya ya Mediteranea likajengwa Sana'a. Utawala wa Kihabeshi ulikwisha 570 Waajemi walipovamia nchi. Hata kipindi chao kikawa kifupi kwa sababu tangu 630 Uislamu ulianza kueneza utawala wake katika Yemeni.

Uislamu wa Sana'a ulifuata mweleko wa Shia tawi la Zaidiya na tangu 1324 utawala ulikuwa mkononi wa maimamu waliorithi cheo. Hata kama watu wa nje walikuwa mabwana wa juu maimamu waliendelea kutawala Sanaa na eneo lake hadi karne ya 20.

Tangu 1516 Milki ya Osmani iliweza kupata ubwana wa juu katika Sanaa ingawa maimamu waliendelea kuwa na athira. Mwaka 1904 Imamu wa Zaidiya Yahya Muhammad Hamid de-Din (1869 - 1948) alifaulu kuwafukuza Waturuki na kuanzisha tena utawala wake kiroho na kisiasa. Baada ya kuporomoka kwa Waosmani katika vita kuu ya dunia ya kwanza alitumia pia cheo cha mfalme. Ufalme huu uliendelea hadi 1962 ulipopinduliwa na jamhuri ya Yemeni ikatangazwa mjini Sana'a.

Utamaduni[hariri | hariri chanzo]

Sana'a ni maarufu duniani kwa ajili ya usanifu wa pekee wa majengo yake. Mji wa kale bado imezungukiwa na ukuta mwenye geti saba. Hasa nyumba za ghorofa zilizojengwa kwa udongo ni maajabu yanayovuta watalii na wataalamu vilevile.

Sana'a iliingizwa na UNESCO katika orodha la urithi wa dunia.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]


Makala hii kuhusu maeneo ya Yemen bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Sana'a kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.