Anwani ya kijiografia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Maelezo ya latitudi na longitudi

Anwani ya kijiografia (pia viwianishi, ing. coordinates) ni namna ya kutaja mahali duniani. Anwani ya kijiografia huelezwa kwa kutaja longitudo na latitudo za mahali fulani.

Dunia hugawiwa katika gredi 360 za longitudo na gredi 180 za latitudo (90° za kaskazini na 90° za kusini).

Latitudo za kaskazini na kusini ya ikweta zinatofautishwa ama kwa kuongeza herufi "N" (=north au kaskazini) na "S" (south au kusini) au kwa alama za "+" (kaskazini) na "-" (kusini).

Gredi za longitudo zinaanza kuhesabiwa kwenye meridiani ya 0° iliyokubaliwa ni mstari kutoka ncha ya kaskazini hadi ncha ya kusini unaopita katika mji wa Greenwich (karibu na London / Uingereza).

Kwa mfano anwani ya National Theater mjini Accra (Ghana) ni: 5°33'14"N (latitudo) na 0°12'2"W (longitudo).

Anwani inaandikwa mara nyingi pia kwa njia ya desimali na hapa inawezekana kutaja mahali kimakinifu zaidi. Hapo viwianishi vya Ikulu mjini Dar es Salaam ni: -6.815592,39.298204.

Matumizi ya anwani ya kijiografia kwenye wikipedia[hariri | hariri chanzo]

Wahariri wengi wanaongeza anwani ya kijiografia katika makala zinazohusu miji, kata, majengo au mahali pengine. Katika wikipedia hii tunaweza kutumia kigezo:coord. Inatosha kunakili mfano kutoka ukurasa wa kigezo hiki na kubadilisha tarakimu zilizopo kwa namba zinazopatikana kwa kutumia Google Earth au ramani nyingine inayoturuhusu kuona anwani ya kijiografia.

Sciences de la terre.svg Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Anwani ya kijiografia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.