Kila mtu anaweza kuhariri makala yoyote, kutoa makosa ya lugha, kutohoa maneno na kuendeleza na kukuza makala, kwa kuandika kwa ufupi au kwa urefu. Tunakushauri ujiandikishe na kufungua akaunti. Angalia Msaada wa kuanzisha makala ili ujifunze unavyoweza kuhariri au kusanifisha ukurasa. Usisite kushiriki; kwa sababu huu ni mradi wa ushirikiano, na hautaisha kamwe. Kamusi elezo itaimarika vizuri zaidi kila wakati. Angalia ukurasa wa jumuia, ukurasa wa jamii, na ule wa makala za msingi za kamusi elezo ili kung'amua unaweza kufanya kazi zipi ili kuboresha Wikipedia.
Wikiindaba 2017 ilikuwa mkutano wa taasisi ya Wikimedia Foundation kwa ajili ya Afrika uliofanyika mjini Accra (Ghana) tarehe 10 - 22 Januari 2017. Waliokaribishwa walikuwa wachangiaji wa Wikipedia pamoja na miradi mingine ya maaarifa huria kutoka nchi za Afrika pamoja na maafisa wa ofisi kuu ya Wikimedia. Shabaha ilikuwa kuimarisha mawasiliano kati ya washiriki na hali ya media huria barani Afrika.
Jina
WikiIndaba ni neno lililoundwa na "Wiki" kwa "Wikipedia / Wikimedia" na "Indaba" ambalo ni neno la lugha la Kizulu yenye maana ya "mkutano, ushauri wa pamoja'. Ilikuwa WikiIndaba ya pili baada ya mkutano wa kwanza uliotokea Afrika Kusini mwaka 2014.
Ng'ombe ni wanyama wakubwa wa jenasi Bos. Spishi ya ng'ombe ina nususpishi au aina nyingi lakini ni spishi moja tu.
Ng'ombe hula manyasi na kutembea kwa vidole viwili.
Asili yake ni aina za ng'ombe wa pori waliofugwa kwa sababu ya nyama na maziwa. Katika nchi nyingi anatumiwa pia kama mnyama wa mizigo anayevuta plau au magari.
Wataalamu huamini ya kwamba aina zote za ng'ombe zina asili katika mashariki ya kati mnamo milenia ya 9 KK ambako watu waliwahi kuwafuga nas kutoka hapa ufugaji ng'ombe ulisambaa kote duniani.
Takwimu ya Wikipedia ya Kiswahili
Idadi ya makala: 40,707
Idadi ya kurasa zote: 93,136 (pamoja na kurasa za watumiaji, majadiliano, msaada n.k.)
(fungua anwani kwa browser yako, badilisha "Mwanzo" kwa jina la makala (hadi makala 10) unayopenda. Unaweza kubadilisha kipindi cha taarifa utakachoona; takwimu kabla ya 2015 hapa)
na makala 100 zilizotazamiwa zaidi "Topviews" kwa kipindi fulani.
(unachagua kati ya makala 100 kwa mwezi au kwa siku)
Jumuia za Wikimedia
Kamusi elezo ya Wiki ni kamusi elezo huru iliyo chini ya Shirika Lisilo la Kiserikali la Wikimedia Foundation, ambalo linasimamia miradi mingine mbalimbali ambayo imeorodheshwa hapo chini. Mpaka sasa miradi inayopatikana Kiswahili ni Wikipedia na Wikamusi. Wikitabu imewekwa Kiswahili lakini bado ni tupu. Mengine inapatikana Kiingereza pamoja na lugha tofauti.