Wikipedia:Jumuia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Lango:Jumuia)
Jump to navigation Jump to search
  • sw: Ukurasa huu ni kwa ajili ya kuwasaidia watu wanaotaka kuboresha kamusi hii na kujadiliana mambo ya jumuiya yetu!

Viungo vya jumuia:

Wikipedia:Sanduku la mchanga Wikipedia:Wakabidhi
Fungua hapa kuona kura kuhusu wakabidhi wapya!
Wikipedia:Makala kwa ufutaji Wikipedia:Makala zinazohifadhiwa Makala zinazotembelewa sana leo hii
Wikipedia:Ubalozi Wikipedia:Kundi la Jenga Wikipedia ya Kiswahili Wikimedia Community User Group Tanzania Wikipedia:Makala zilizoombwa Angalia michango ya watumiaji
  • en: Welcome to the Swahili Wikipedia village pump!

Kumbukumbu ya miaka iliyopita

Majadiliano ya awali yamehamishiwa hapa:

Jenga Wikipedia ya Kiswahili

Kwa wote wanaopenda kutafakari na kujadiliana nasi namna ya kuendeleza wikipedia hii ya Kiswahili wakabidhi walianzisha kundi la meta:Jenga Wikipedia ya Kiswahili. Unaweza kujiandikisha pale kama umehariri hapa kwa muda wa mwaka moja angalau.

Changamoto ya wahariri wapya, kampeni za kuunda makala

Wapendwa,

ilhali niko safarini siku hizi nimepita kazi ya wachangiaji wa zoezi la miji ya Tunisia. Nimeona makosa mazito na makala nyingi ambayo ni mbaya. Nimeanza kuzuia wachangiaji wanaorudia kumwaga google translate bila kusoma matokeo yake. Kipimo changu ni, kama Kiswahili hakieleweki, au kichekesho tu (mara kadhaa: mji fulani ilikuwa "raia" wa kirumi..., kwa sababu google translate haijui "civitas" ni nini na wachangiaji hawajali), basi hakusoma anachopakua.

Ninaomba tutafute nafasi ya kushauriana kati ya wakabidhi kwa njia ya mkutano wa google meetup au zoom. Naona idadi ya makala mbaya imeanza kuzidi, na kazi ya kusafisha inazidi. Ninapendekeza kupatana kuhusu hatua ya kusimamisha wachangiaji wanaoopuuza kanuni. Na pia jinsi ya kuongoza wachangiaji wapya wakati wa kampeni hizo wakileta matokeo katika swwiki.

Nikimzuia mtu, namweleza kwamba anaweza kupeleka malalamiko kwenye ukurasa wa jamii. Ninamwomba pia aniandikie kwenye ukurasa wangu wa majadiliano na kusema kama yuko tayari kusahihisha kurasa zake (ambako ningempa mwongozo). Akiandika, nitaondoa zuio. Kama la, basi. Akionyesha anajaribu kusahihisha arudi.

Kuhusu mazoezi ya kutunga makala naona kwanza yaandaliwe vizuri zaidi. Mfano jamii, interwiki, viungo vya ndani vielezwa na kuandaliwa pia. (hapa tumepata miji ya leo ya Tunesia ambayo yamepangwa katika jamii ya kiakiolojia pekee).

Pendekezo : wageni wote wasipakue moja kwa moja. Kila moja aweke makala zake kwenye ukurasa wake mwenyewe, mfano "mtumiaji:Kipala/1/Sousse". Mwisho wa KILA KIPINDI majirani wasome makala za jirani. Waongee kifupi na kuuliza maswali au kudokeza kasoro. Baada ya masahihisho makala yapelekwe kwenye name space kama "Sousse". KAMWE MAPEMA!