Majadiliano ya mtumiaji:Idd ninga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Twamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo - hata kuitafsiri kutoka katika Wikipedia kwa lugha nyingine. Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wa sanduku la mchanga. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike pekee kwenye ukurasa wako wa mtumiaji baada ya kufungua akaunti. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho. Ujue miiko: usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje wala matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo). Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!

Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non speaker better first communicate with one of our admins who will advise you. You find them at Wikipedia:Wakabidhi. And btw: NEVER post computer translated texts (like google-translate, mediawiki Content Translation etc.) nor copied texts/images from other webs to this site! And do not use links to commercial pages. As a newcomer we advise that you register your email which will not be visible to others but it allows to contact you, which often is helpful in case of problems.

Kutaja vyanzo[hariri chanzo]

Ndugu nimeona ulileta makala ambazo nilipeleka katika ukurasa wetu ambako zitaangaliwa kama zinaweza kubaki au la. Angalia Wikipedia:Mwongozo_(Anzisha_makala) na hasa Wikipedia:Umaarufu . Sitaki kukukatisha tamaa, ukiwa na swali: karibu! Kipala (majadiliano) 14:11, 25 Agosti 2018 (UTC)

Asante sana kwa bahati hii ya pekee ya kuweza kuleta historia na wasifu wa washairi na waandishi wa VITABU Tanzania.

naomba tuendelee kuvumiliana kidogo katika kipindi himi kwani kuna baadhi ya makosa ya kiuandishi hutokea.

naweza kuwasiliana nanyi moja kwa MOJA moja kwa barua pepe yangu ?
Sawa kabisa, ukienda ukurasa wangu utaona upande wa kushoto chini ya kichwa "Vifaa" kipengele "Email this user", hapa utanipata. Kipala (majadiliano) 13:28, 26 Agosti 2018 (UTC)

Saadani Abdu Kandoro[hariri chanzo]

Asante kwa mchango kuhusu Saadani Kandoro, ni muhimu. Ila tu hatuwezi kuacha makala bila vyanzo na marejeo. Ulipata wapi matini zako? Lazima kutaja. Kipala (majadiliano) 12:58, 16 Septemba 2018 (UTC)

JASHO LA MVUA[hariri chanzo]

Umeleta makala hii, mimi napendekeza kuifuta (lakinii una nafasi ya kuiboresha. Matini uliyoleta haifuati muundo wa makala, haitaji nani ni mwandishi na haielezi yaliyomo ya kitabu. Badala yake unaleta matini ya tangazo la biashara ya wachapiaji ambayo haikubaliki. Tumia muda unaobaki kabla ya kufutwa kwa makala!. Kipala (majadiliano) 19:57, 20 Aprili 2019 (UTC)

Patrick Mfugale[hariri chanzo]

Asante kwa mchango huu wa maana. Ila tafadhali sana usimalize haraka. Jitahidi kuchungulia sentensi zako, na kuepukana na yale makosa mengi ya tahajia. Asante. Kipala (majadiliano) 21:05, 9 Februari 2020 (UTC)

Kuboresha makala[hariri chanzo]

Ndugu, tunakushukuru kwa michango yako, ila angalia tunavyoirekebisha iwe bora zaidi. Naona unarudia makosa yaleyale, kumbe unaweza kutupunguzia kazi ya kuyarekebisha. Pembeni mwa mabadiliko ya karibuni angalia tofauti kati ya ulivyoandika wewe na ninavyorekebisha mimi. Wote tumejifunza hivi. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 06:31, 27 Februari 2020 (UTC)

Mlima Kubi Gangri[hariri chanzo]

Asante kwa makala. Tafadhali maliza makala! Haina jamii, haina interwiki (kuunganisha na lugha nyingine). Pia inafaa kuangalia makala ya en.wiki na angalau kunakili kutoka pale vyanzo na marejeo. Kama una swali, uliza - usikae kimya. Hakuna maswali mabaya, lakini kuna makala mabaya shauri ya kutouliza swali! Kipala (majadiliano) 18:39, 5 Machi 2020 (UTC)

Kinachokosekana ni jamii na interwiki.
Jamii: kwanza angalia makala ya enwiki inatumia jamii gani (kama makala ya enwiki ipo). Pale unaona "Categories: Mountains of Nepal,Mountains of the Tibet Autonomous Region,China–Nepal border,International mountains of Asia,Nepal geography stubs,Tibet geography stubs". Hapa utachagua, Hatuna jamii kuhusu mpaka ule, ningeacha. Vilevile hatuna "milima ya kimataifa..". Lakini nisipokosei tuna milima ya Nepal (kama bado: jiografia ya Nepal?), pia milima ya Tibet (?) au China. Lazima uangalie. Hakika tuna jamii:Himalaya. Inafaa. Hizi za "stubs" (=mbegu za...) mimi mwenyewe sianzishi kama haziko tayari.
Interwiki: tafuta jina la makala kwa Kiingereza. Halafu kwenye ukurasa wa makala mpya "Mlima Kubi Gangri" bofya chini kushoto hapa "Lugha - Ongeza viungo/Add links". Sasa fuata maelezo ya hapa: Wikipedia:Mwongozo_(Viungo_vya_Wikipedia).
Menginevyo ningeshauri fungua makala ya Kiingereza. Hatuwezi (bado) kunakili hiyo infobox na pia hatuwezi kuchukua ramani hii. Lakini unaweza kuchukua majiranukta. Bofya "Edit Source". Fungua pembeni makala ya Mlima Everest, bofya hariri chanzo, nakili sehemu yote ya majiranukta (coordinates), bandika ktk makala ya Mlima Kubi Gangri, sasa chukua namba kutoka coordinates ya enwiki na andika katika sehemu uliyonakili kutoka Everest.

Pia nakili sehemu ya "External links" kutoka enwiki, bandika sw. BAsi hii itoshe nitaangalia kesho ulifika wapi. Wasalaam. Kipala (majadiliano) 19:22, 5 Machi 2020 (UTC)

Mtumiaji:Idd Ninga[hariri chanzo]

--Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:39, 22 Aprili 2020 (UTC)Salamu, Hongera kwa kuendeleza michango yko katika sw.wiki ni vyema uandike chochote katika ukurasa wako wa mtumiaji. 196.41.58.174 19:10, 11 Machi 2020 (UTC)

Idd habari naomba uwasiliane nami kwa barua pepe kupitia "email this user" ukiangalia ukurasa wangu wa mtumiaji (bofya chini kwa jina langu, menyu "Vifaa" upande wa kushoto, nafasi ya sita kwenye menyu ).
Tukiwasiliana kwa email kupitia wikipedia, anwani haionyeshwi kwa hiyo ni siri yako na yangu.
Naona unafanya mengi na hapa nafurahi. Naona pia unahitaji bado ushauri maana kuna kasoro ambazo si lazima, sina shaka kwamba unaweza kushika haraka na kuboresha makala zako. Kipala (majadiliano) 16:53, 14 Machi 2020 (UTC)

Tangazo[hariri chanzo]

Habari ndugu Mwanawikipedia!

Mimi ni mwezeshaji wa mradi uitwao Mwongozo Wa Kimataifa Wa Mwenendo Na Maadili. Ni mradi mchanga/mpya ambao Shirika la Wikimedia Foundation linanuia kuuanzisha endapo wadau wataona ni mradi unaofaa. Nakukaribisha usome mwongozo huo na kisha utoe maoni yako kwa kujibu maswali yote au baadhi yake kwa yale utakayopenda kuyatolea maoni HAPA

Taarifa zaidi kuhusu Mwongozo wa Kimataifa wa Nidhamu na Mwenendo

Shirika la Wikimedia Foundation lina mpango wa kuanzisha Mwongozo Wa Kimataifa Wa Mwenendo Na Maadili. Lengo la mwongozo huo ni kujaribu kuainisha vitu vya msingi vinavyopatikana katika miongozo midogo midogo iliyopo tayari katika kila jamii husika (mfano Jumuiya yetu hii ya wahariri wa Wikipedia ya Kiswahili). Lengo hasa la mwongozo huu ni kutengeneza mazingira ambayo wanawikipedia wote duniani watakuwa na uelewa wa pamoja juu ya vitu vya msingi kuhusu nini kinakubalika na kipi hakikubaliki wakati wa uchangiaji (uhariri) wa Wikipedia na pale wanawikipedia wanapowasiliana kwenye Wikipedia au ana kwa ana katika warsha na mikutano ya Wanawikipedia. Wazo hilo limekuja baada kukithiri kwa baadhi ya Wanawikimedia kukumbana kufanyiwa unyanyasaji wa kitabia (mfano matusi, kuitana majina yasiyofaa, kutishiana n.k) na Wanawikimedia wenzao, hivyo kuwakatisha tamaa ya kuendelea kuchangia katika miradi ya Wikimedia.Hivyo, wewe kama mdau muhimu katika miradi ya Wikimedia Foundation, unakaribishwa ku soma zaidi kuhusu mwongozo huo Hapana baada ya kuusoma mwongozo huo unaweza ku toa maoni yako Hapa kabla ya tar 15 April 2020.

Mwaliko wa kujiunga na kundi la Wahariri wa Wikipedia

Nakukaribisha ujiunge na kundi la Wahariri wa Wikipedia kutoka Dar es Salaam ili tuweze kujadiliana na kubadilishana uzoefu na mambo kadha wa kadha kuhusu Uhariri wa Wikipedia. Iwapo utapenda kujiunga, usisite kuwasiliana nasi kupitia wikitzagroup@gmail.com, na kwa taarifa zaidi kuhusu kundi la Wahariri wa Wikipedia wa hapa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla na miradi waliyoitekeleza tayari, unaweza tembelea hapa ukurasa wao wa meta uitwao Wikimedia Community User Group Tanzania au pia katika Facebook kwa jila la Wikimedia Tanzania.

Ndimi AMtavangu (WMF) (majadiliano) 17:44, 5 Aprili 2020 (UTC)

Makala za lugha[hariri chanzo]

Hongera kwa juhudi zako! Mradi unapenda mambo ya lugha, angalia kazi niliyofanya leo ya kurekebisha majina ya lugha nyingi yaliyokosewa upande wa ngeli: Ki- ya badala ya Ki- cha. Karibu kurasa zote nimehamisha juu makala. Sasa naomba wewe urekebishe makala yenyewe kulingana na kichwa kipya. Ukikuta k.mf. Kiswahili ya kisasa, weka Kiswahili cha kisasa. Asante na amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:39, 22 Aprili 2020 (UTC)


Kupanusha makala za Tanzania[hariri chanzo]

Idd Habari zako, naona siku hizi unakazia makumbusho, asante sana. Ilhali unapenda kuchangia na unachapa kazi, nina pendekezo: isingekuwa vibaya kupanusha makala zetu kuhusu Tanzania na Kenya, yaani nchi ambako wasomaji wetu wengi wanaishi. Labda uangalie en:Category:Tanzania. Hapa kuna makala mengi ambayo yanafaa kupelekwa swwiki. Kwa kawaida inasaidia kuanza na jamii ndogo (subcategory) fulani. Maana insaidia kuzoea msamiati wa pekee unaorudiwa, mfano ukianza na en:Category:Economy of Tanzania. Faida yake ni mara nyingi makala hizi zina marejeo tayari. Tahadhari ni: mara nyingi makala si za kisasa, (mfano: kama mkurugenzi wa kampuni anatajwa, au mwanasiasa anatajwa ni waziri, kumbe siyo tena au ameshakufa...), hapa inafaa kuchungulia haraka ka google na kuhakikisha kama ni bado.

Unaonaje? 197.250.228.130 07:35, 6 Mei 2020 (UTC)

Uteuzi kuwa mkabidhi[hariri chanzo]

Salaam! Ulipendekezwa na kukubaliwa kupata haki za mkabidhi. Je, uko tayari kupokea uteuzi huu na kushiriki katika kazi mara kwa mara kama jinsi ilivyoelezwa katika ukurasa wa wakabidhi? Tunaomba jibu lako kwa baruapepe katika wiki hii. Tumia zana za Wikipedia kutuma barua pepe. --'Muddyb Mwanaharakati' 'Longa' 07:44, 13 Septemba 2020 (UTC)

We sent you an e-mail[hariri chanzo]

Hello Idd ninga,

Really sorry for the inconvenience. This is a gentle note to request that you check your email. We sent you a message titled "The Community Insights survey is coming!". If you have questions, email surveys@wikimedia.org.

You can see my explanation here.

MediaWiki message delivery (majadiliano) 18:54, 25 Septemba 2020 (UTC)