Msaada:Picha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Picha zinapendezesha, lakini si mapambo tu ya makala, bali zinasaidia pia kuelewa vizuri zaidi jambo linajojadiliwa katika makala. Ukurasa huu unakusaidia kuchagua na kuingiza picha katika makala.

Ujue ya kwamba tunatumia picha kutoka Wikimedia Commons tu. Ni marufuku kutumia picha "kutoka intaneti", google au mitandao ya kijamii.

Viungo vya picha

Picha au michoro huonekana katika makala kwa njia ya viungo. Ili picha ionekane lazima kwanza faili yake iwepo katika kumbukumbu ya Wikipedia. Hapa kuna njia 2:

1) kutumia akiba kubwa sana ya faili za picha huria zilizopo tayari katika kumbukumbu ya sw.wikipedia.org au commons.wikimedia.org au
2) kupakia faili ya picha kutoka kompyuta yako. Kwa kupakia unaingiza picha hiyo katika kumbukumbu ya Wikipedia. Kabla ya kufanya hiivyo sharti kuhakikisha ya kwamba una haki ya kufanya vile. (tazama chini: wapi kuchukua picha za kupakiza).
Nembo ya Tanzania 250px
maandishi ya kiungo chake ni
Picha:Coat of arms of Tanzania.svg|thumb|200px|Nembo ya Tanzania 250px

Umbo la kiungo cha picha

Kuna njia mbalimbali za kuingiza picha. Hapa sw:wikipedia tufuate mtindo wa "thumbnail" au kifupi "thumb". Umbo la "thumb" lina faida mbalimbali na kuepukana na matatizo ya picha kubwa mno.

Kiungo cha picha ina sehemu nne ndani ya mabano mraba zinazotenganishwa kwa alama ya "|" inaonekana hivyo:

[[Picha:JINA LA PICHA|thumb|NAMBA YA UPANApx|MAELEZO YA PICHA]] 
 1. sehemu 1 - JINA: Jina la picha sharti ni sawa kabisa na jina la faili yake. Inatanguliwa na neno "Picha:". Badala ya picha programu inapokea pia "faili" au maneno ya Kiingereza "image" na "file".
 2. sehemu 2 - THUMB: neno hili "thumb" sharti ifuate. Maelezo haya yafaa kwa umbo hili pekee.
 3. sehemu 3 - NAMBA + px: namba inaonyesha upana wa picha katika makala. Namba hii kwa kawaida iwe kati ya 80px na 300px. "px" ni kifupi cha "pikseli". Usichague picha kubwa mno kwa sababu picha kubwa zinachelewesha makala kuonekana dirishani. Uhurumie wenzetu wenye intaneti mwenda polepole! Hapa ni vema kufanya jaribio kwa kutumia kibonye cha "Onyesha hakikisho la mabadiliko" kabla ya kuhifadhi kabisa na hapa unaweza kucheza kidogo na kuona ipi inafaa. Mtazamaji akitaka kuona picha kubwa ataigonga tu itatokea kubwa kabisa. Angalizo: Ukiacha sehemu hii ya tatu itaonekana kwa upana sanifu ya 180px.
Tofauti hapa ni yafuatayo: thumb|100px|left| inayopeleka picha upande mwingine
4 sehemu 4 MAELEZO: Kama unaandika maelezo jinsi unavyopenda lakini usiandike maelezo marefu mno!

Picha upande wa kushoto

Mfumo wa "thumb" unaweka picha upande wa kulia. Ukitaka ionekane upande wa kushota uningiza "left|" kama sehemu ya 5 ndani ya maandishi ya kiungo kabla ya maelezo.

Mkusanyo wa picha (gallery)

Wakati mwingine inafaa kuingiza mkusanyo wa picha kuhusu mada fulani. Linganisha makala ya Tongoni.

Hapa tunatumia alama hizi (unaweza kunakili sehemu hii na kuitumia katika dirisha la "Hariri chanzo", kwa kuweka majina na maelezo yenyewe)

<gallery>
Jina la picha.jpg|Matini chini ya picha (si lazima)</br>
Jina la picha.jpg|Matini chini ya picha (si lazima)</br>
Jina la picha.jpg|Matini chini ya picha (si lazima)
</gallery>

Kuna fomati zaidi, soma hapa en:Help:Gallery_tag

Wapi kupata picha

Picha za Wikipedia

Yaliyomo yote katika Wikipedia pamoja na picha yamewekwa kwenye uwanja wa umma, yamekuwa mali ya umma. Uko huru kutumia yote yaliyomo kwenye miradi ya Wikipedia.

Katika makala nyingine

Ukiona picha kwenye makala nyingine ya sw:wikipedia, au kwa mfano katika makala ya Kiingereza unayotafsiri, unaweza kunakili kiungo chake.

 1. Bofya "hariri"
 2. Tafuta kiungo cha picha unayotaka; nakili kiungo chote (au jina la picha pekee pamoja na nyongeza kama vile ".jpg")
 3. Mwaga katika makala yako ya sw:wikipedia
 4. Sahihisha umbo la kiungo jinsi inavyohitajika (en:wikipedia hawatumii wakati wote umbo la "thumb" - hapa sharti uingize; wikipedia za lugha nyingine wana majina mengine kwa "picha" zisizotambuliwa kwetu kwa mfano "Bild:" n.k.; sharti usahihishe na kubadilisha)
 5. Jaribisha kama picha inaonekana kwa njia ya "onyesha hakikisho.."; kama haionekani: tazama chini!

Katika makala za en:wikipedia

Watumiaji wengi watachungulia pia Wikipedia ya Kiingereza na kuona picha huko. Hapa kuna aina mbili za picha:

 1. Picha kutoka Commons.wikimedia: hii ni kumbukumbu kubwa sana ya wikimedia na jina la faili hapa inasomeka katika miradi yote ya wikimedia pamoja na wikipedia pia kwetu.
 2. Picha inayopatikana katika wikipedia ya Kiingereza tu. Picha hii haitaonesha mpaka umeichukua na kuingiza katika wikipedia yetu.
  1. Kuna sababu kadhaa za picha kutokuwepo katika commons. Kwa mfano mtumiaji huko aliona ugumu kuzoea commons lakini amezoea kupakiza kwenye en:wikipedia. Kwetu sw:wikipedia kuna picha na ramani yenye maandishi yaliyoswahilishwa mara nyingi hazikupelekwa commons maana wengine hawaelewi. Sababu nyingine ni hakimiliki; nchi zenye sheria za Marekani na Uingereza zina utaratibu wa kutumia picha zisizokubalika katika nchi nyingine kwa hiyo picha hizi haziwekwi commons kwa matumizi kote duniani. (Hapa sw:wikipedia tunaweza kutumia picha zote kutoka en:wikipedia).
  2. Kama picha haiko commons lakini katika wikipedia ya lugha fulani kuna njia ifuatayo:
  3. Bofya kwa kibonye cha kulia cha puko kwenye picha, chagua "save as" na uihifadhi kwenye kompyuta yako (kwa muda, futa baadaye).

Halafu utapakia picha yako hapa fuata maelezo hapo chini "Kupakia picha".

Kutoka Commons moja kwa moja

Commons ni mahali pakubwa sana. Unapata chaguo kweli. Picha ziko pamoja katika vikundi vya "Categories". Njia rahisi ya kuingia ni:

 1. Ukiona picha ya kufaa lakini unataka picha nyingine kuhusu mada hiyohiyo bofy kwenye picha.
 2. Faili ya picha inafunguliwa, chini yake kuna maneno "Faili hili linatoka Wikimedia Commons. Maelezo yapo kule kwenye ukurasa wake wa maelezo unaonekana hapo chini."
 3. Bofya maneno mazito "ukurasa wake wa maelezo" utafika kwenye ukurasa wa faili kwenye commons.
 4. hapa angalia chini kabisa utaona kasanduku inayosema Categories (mfano wetu: Categories: Coats of arms of Tanzania | Fire and containers in heraldry .....). Hapa unaingia na utaona mifano mingine (kama ipo).

Picha kutoka nje ya Wikipedia?

Hapa lazima kuwa waangalifu maana katika Wikipedia hatutaki matatizo ya kisheria. Tunaheshimu hatimiliki za picha!

Kuomba hakimiliki

Ukimjua mwenye hakimiliki ya picha (mpiga picha, mchoraji wa taswira/katuni) unaweza kumuomba kibali cha kwamba kazi yake ipelekwe kwenye laiseni huria. Soma mifano ya barua unayoweza kuandika, na barua / email itakayohitajika kutoka mwenye hakimiliki hapa: en:Wikipedia:Example_requests_for_permission.

Kutoka google-search?

Hapana! Kwa kawaida picha zinazopatikana kwa njia ya Google hazifai wa sababu hakimiliki si huru. Hazikubaliki kwenye Wikipedia. Isipokuwa kama picha kwa hakika ina umri mkubwa na wote wenye hakimiliki ya picha hiyo wameshakufa tangu miaka 70. Tazama chini!

Mali ya umma?

Angalia ukurasa huu katika en:wikipedia wanapoorodhesha picha ambazo zimekuwa mali ya umma: Public Domain Image resources

Picha zangu?

Hii ni sawa kama hakuna haki za wale wanaoonyeshwa kwenye picha hii (au haki ya kile kinachoonyeshwa, mfano picha ya taswira). Fuata maelezo ya juu "Katika makala za en:wikipedia" yaani hifadhi kwanza kwenye kompyuta yako halafu pakia. Kwenye nafasi ya hatimiliki utachagua "Own work, all rights eleased". Kwenye nafasi ya maelezo utaandika umechukua picha wapi na lini na kwa nini hakuna haki wa wale wanaoonekana (kwa mfano: wamekubali, au: ni picha ya barabarani).

Lakini tahadhari: usishangae ukiulizwa tena - maswali yale hayawezi kuelezwa hapa katika mistari miwili!

Dirisha la kupakia (bofya hapa ukitaka kuona mfano kwa karibu zaidi)

Kupakia picha

Baada ya kuhakikisha ya kwamba picha uliochagua ni halali kuingizwa katika wikipedia unahitaji kuipakiza ("upload"). Kabla ya kuipakiza utahifadhi picha kwenye kompyuta yako. Huwezi kuchukua picha kutoka intaneti moja kwa moja na kuipeleka wikipedia.

Fuata hatua hizi:

 1. Hifadhi picha ulioteua kwenye kompyuta yako.
 2. hakikisha ya kwamba picha ina moja kati ya fomati zifuatazo: png, gif, jpg, jpeg, xcf, pdf, mid, ogg, ogv, svg, djvu, oga. Kama si vile, fungua kwa programu ya picha na hifadhi tena katika fomati kama .png au .jpg.
 3. Katika dirisha la wikipedia bofya "pakia faili" halafu katika dirisha jipya bofya "Search" yaani unaelekea kwenye kompyuta yako penye faili uliyohifadhi, lazima ionekane mwishowe katika nafasi ya "Jina la faili la chanzo"
 4. Kwenye nafasi ya "Jina la faili la mwishilio" unaweza kubadilisha jina jinsi litakavyoonekana katika sw:wikipedia
 5. Kwenye nafasi ya Hatimiliki unachagua ile inayofaa. Ukichukua kutoka en:wikipedia utaweka "GNU Free Documentation License". KAMA kuna maelezo yenye masharti chagua "GDFL content with disclaimers...". Kama ni picha yako, tazama juu. Menginevyo uliza wakabidhi!
 6. Kwenye nafasi ya muhtasari weka anwani asilia ya faili kwa mfano "Kutoka http://en.wikipedia.org/wiki/Image:Coat_of_arms_of_Tanzania.svg. Kama umeswahilisha ramani n.k. ongeza "imebadilishwa na user: JINA LAKO". Kama ni picha uliopiga mwenyewe taja tarehe na mahali pa picha, mengine soma juu!
 7. Ingiza kiungo kwa jamii ya picha katika mstari mpya kwenye nafasi ya muhtasari. Chagua jamii husika ukianza kuchungulia kwenye [[Jamii:Picha za Wikipedia]]. Weka jina la jamii katika mabano mraba jinsi ilivyo mbele kwa Jamii:Picha za Wikipedia.
 8. Mwishowe bofya "Pakia faili".