Tongoni
Tongoni ni kata iliyopo ndani ya eneo la Jiji la Tanga katika Mkoa wa Tanga, Tanzania yenye Postikodi namba 21207.
Kata ina ukubwa wa kilomita za mraba 44 ( maili 17),[1] pia ina mwinuko wa wastani wa mita 30 (futi 98),[2]
Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ina wakazi wapatao 4,594 [3][4] waishio humo.
Tongoni iko takriban kilomita 14 upande wa kusini wa kitovu cha jiji kando ya barabara inayokwenda Pangani, ikitazama Bahari Hindi.
Magofu ya Tongani yanapatikana katika kata ya Tongani, mji wa Waswahili enzi za mawe za kati. Mahali pa kihistoria jinsi inavyoonekana leo kuna msikiti na takriban makaburi 20.[5] Takriban miaka 600 iliyopita kulikuwepo hapa mji wa Tangata (pia: Mtangata) iliyokuwa mahali muhimu pa biashara. Mahali pake kwenye mdomo mpana wa mto unaoishia hapa palileta nafasi salama ya kutia nanga kwa jahazi. Inasemekana ya kwamba nahodha Mreno Vasco da Gama alipumzika hapa kidogo wakati wa safari yake ya kwanza kuelekea Bara Hindi mnamo mwaka 1498. Magofu ni pamoja na msikiti na makaburi yenye nguzo jinsi ilivyokuwa kawaida kwenye makaburi ya Waswahili.[6]
Magofu ya Tongoni[hariri | hariri chanzo]
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- ↑ https://www.citypopulation.de/en/tanzania/northern/admin/
- ↑ https://elevationmap.net/tongoni-tanga-tz-1012567430
- ↑ Sensa ya 2012, Tanga - Tanga CC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-05-16.
- ↑ http://tanzania.countrystat.org/fileadmin/user_upload/countrystat_fenix/congo/docs/Census%20General%20Report-2012PHC.pdf
- ↑ Tongoni Ruins, tovuti ya Lonely Planet, iliangaliwa Septemba 2018
- ↑ Briggs, McIntyre ukurasa 372
Vitabu[hariri | hariri chanzo]
- Philip Briggs, Chris McIntyre: Tanzania Safari Guide: With Kilimanjaro, Zanzibar and the Coast, Bradt Travel Guides 2013, ISBN-10: 9781841624624, ISBN-13: 978-1841624624ISBN
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Tongoni kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |
![]() |
Kata za Wilaya ya Tanga - Tanzania | ![]() |
---|---|---|
Central • Chongoleani • Chumbageni • Duga • Kiomoni • Kirare • Mabawa • Mabokweni • Magaoni • Majengo • Makorora • Marungu • Masiwani • Maweni • Mnyanjani • Msambweni • Mwanzange • Mzingani • Mzizima • Ngamiani Kaskazini • Ngamiani Kati • Ngamiani Kusini • Nguvumali • Pongwe • Tangasisi • Tongoni • Usagara |