Kata

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

--Kwa kata kama jina la ngazi ya utawala tazama kata (eneo)--

Kata ni chombo maalum kitumiwacho na makabila mengi nchini Tanzania, hasa na Wachagga huko mkoani Kilimanjaro. Kata hutumika kunywea pombe iitwayo mbege.

Matengenezo[hariri | hariri chanzo]

Kata hutengenezwa kwa kutumia matunda jamii ya tikiti yaitwayo vibuyu. Matunda haya hukatwa katikati kisha hutolewa nyamanyama za ndani ili kupata uwazi ambao baada ya tunda kukaushwa hupatikana aina ya kikome kizito ama kwa jina kibuyu. Kikombe hiki kikiisha kukauka hutobolewa kwa upana matundu mawili ambayo hukobekwa kijiti kirefu kitumikacho kama mshikio wa kata.