Chongoleani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Chongoleani ni kata ya Tanga Mjini katika Mkoa wa Tanga, Tanzania, yenye Postikodi namba 21205.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 5,882 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ina wakazi wapatao 4,737 [2] waishio humo.

Kutokana na mpango wa serikali wa usambazaji umeme vijijini, Chongoleani ni moja ya kijiji kilichopo kwenye wilaya ya Tanga mjini ambacho kimefaidika na huduma ya umeme toka mwaka 2015, kwa sasa karibu nusu ya wakazi wake wana huduma ya umeme.

Kwa upande wa huduma ya maji bado wanategemea maji ya visima na kutokana na wakazi wake wengi kukosa huduma ya vyoo inapelekea maji ya kisima kuwa si salama sana.

Shughuli kubwa ya uchumi ni uvuvi wa samaki, ukulima wa chumvi na kwa kiasi kidogo ukulima wa mazao ya chakula kama mihogo na mchele na ufugaji wa wanyama kama mbuzi, kuku na ng`ombe.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. "Sensa ya 2012, Tanga - Tanga CC". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-05-16. 
Kata za Wilaya ya Tanga - Tanzania

CentralChongoleaniChumbageniDugaKiomoniKirareMabawaMabokweniMagaoniMajengoMakororaMarunguMasiwaniMaweniMnyanjaniMsambweniMwanzangeMzinganiMzizimaNgamiani KaskaziniNgamiani KatiNgamiani KusiniNguvumaliPongweTangasisiTongoniUsagara


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Chongoleani kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.