Mfumo wa Msimbo wa Posta Tanzania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Postikodi Tanzania)
Mfano wa matumizi ya Msimbo wa Posta katika anwani ya barua (alama nyekundu)

Mfumo wa Misimbo ya Posta ya Tanzania (postikodi Tanzania) umeanzishwa tangu mwaka 2012. Msimbo wa posta ni namba iliyochaguliwa kwa kila kata nchini. Kila kata ina msimbo wa tarakimu tano.

Nia ni kuwa kila barua inayotumwa nchini Tanzania ionyeshe namba hiyo juu ya bahasha yake kama sehemu ya anwani ya barua au kifurushi ili kurahisisha na kuharakisha usafirishaji.

Namba ya msimbo wa posta ni tofauti na namba ya sanduku la posta; msimbo wa posta unahusu mahali au eneo, ilhali sanduku la posta linamhusu mpokeaji wa barua.

Muundo wa tarakimu katika msimbo wa posta wa Tanzania

Msimbo wa posta nchini Tanzania huwa na tarakimu tano zilizopangwa kufuatana na ngazi za utawala wa nchi:

  • tarakimu ya kwanza inaonyesha kanda
  • tarakimu ya pili (pamoja na inayotangulia) inaonyesha mkoa
  • tarakimu ya tatu (pamoja na zinazotangulia) inaonyesha wilaya au halmashauri
  • tarakimu za nne na tano (pamoja na zinazotangulia) zinaonyesha kata.
    • Badala ya kata tarakimu kamili zinaweza kuteuliwa pia kwa ajili ya mteja mkubwa anayepokea barua nyingi sana, au eneo maarufu au shughuli maalumu. Mfano ni kampuni kubwa au wizara kuwa na msimbo wa pekee.
    • Hakuna misimbo ya pekee kwa kata zote za Tanzania; wakati mwingine kata kadhaa za wilaya ileile zimeunganishwa kwa kazi ya posta na kuwa na msimbo mmoja[1]

Mfano:

6 5 4 0 1 ni msimbo wa posta kwa Kilwa Masoko.
6 ni tarakimu kwa Kanda ya Pwani
6 5 inaonyesha Mkoa wa Lindi
6 5 4 inataja Wilaya ya Kilwa (651 ni Lindi mjini, 563 Nachingwea, 655 Liwale, na kadhalika)
• Tarakimu za mwisho 0 1 ni za kata ya Kilwa Masoko.

Ilhali wilaya ya Kilwa huwa na kata 21, misimbo ya kata za Kilwa inaendelea kuanzia 6 5 4 0 1 (Kilwa Masoko) hadi 6 5 4 2 1 (Kibata).

Maana yake kama barua inaonyesha anwani ya „65421 Kibata“ inaweza kusafirishwa, si lazima mfanyakazi aulize Kibata iko wapi? Inatosha akijua ni barua kwenda pwani („6“) na Mkoa wa Lindi („65“). Pale Lindi wanajua wilaya zao na 654 ni Kilwa, vivyo hivyo hao wanajua kata katika eneo lao.

Utaratibu huo unatunza nafasi kwa kuanzishwa kwa vitengo vipya; kanda linaweza kuongezwa mikoa hadi 10, kila mkoa wilaya hadi 10, na kata hadi 100 kila wilaya. Kuna pia nafasi kwa kanda mpya 2.

Kanda

Kanda ni hizi zifuatazo, na kila mkoa wa Tanzania ni sehemu ya kanda fulani:

  1. Dar es Salaam (Ilala, Kinondoni, Temeke, Ubungo, Kigamboni)
  2. Kaskazini
  3. Ziwa
  4. Kati
  5. Nyanda za Juu Kusini
  6. Pwani
  7. Zanzibar

Ugawaji wa misimbo ya posta kwenye mikoa na wilaya

1. Kanda ya Dar es Salaam

Eneo Tarakimu Mfano wa msimbo wa kata
Mkoa wa Dar es Salaam 11
Manisipaa ya Ilala 11, 12 Kivukoni 11101
Manisipaa ya Kinondoni 14 Magomeni 14101
Manisipaa ya Temeke 15 Temeke 15101
Manisipaa ya Ubungo 16 Mburahati 16101
Manisipaa ya Kigamboni 17 Kimbiji 17101

2. Kanda ya Kazkazini

Eneo Tarakimu Mfano wa msimbo wa kata
Mkoa wa Tanga 21
Mji wa Tanga 211,

212

Central 21101

Tangasisi 21201

Wilaya ya Pangani 213 Bushiri 21307
Wilaya ya Muheza 214 Majengo 21401
Wilaya ya Mkinga 215 Daluni 21501
Mji wa Korogwe 216 Manundu 21601
Wilaya ya Korogwe 216 Mashewa 21627
Wilaya ya Lushoto 217 Sunga 21723
Wilaya ya Handeni 218 Kabuku 21815
Mji wa Handeni 218 Chanika 21801
Wilaya ya Kilindi 219 Songe 21901
Mkoa wa Arusha 23
Mji wa Arusha 231 Sekei 23101
Wilaya ya Arusha 232 Olturumet 23201
Wilaya ya Meru 233 Usa River 23301
Wilaya ya Monduli 234 Monduli Mjini 23401
Wilaya ya Longido 235 Longido 23501
Wilaya ya Karatu 236 Karatu 23601
Wilaya ya Ngorongoro 237 Orgosorok 23701
Mkoa wa Kilimanjaro 25
Manisipaa ya Moshi 251 Mawenzi 25101
Wilaya ya Moshi 252 Mabogini 25201
Wilaya ya Siha 254
Wilaya ya Hai 253 Machame Mashariki 25301
Wilaya ya Mwanga 255 Jipe 25501
Wilaya ya Same 256 Same 25601
Wilaya ya Rombo 257 Mahida 25701
Mkoa wa Manyara 27
Mji wa Babati 271 Babati 27101
Wilaya ya Babati 272 Magugu 27201
Wilaya ya Hanang 273 Katesh 27301
Wilaya ya Mbulu 274 Ayomohe 27401
Wilaya ya Kiteto 275 Kibaya 27501
Wilaya ya Simanjiro 276 Orkesumet 27601

3. Kanda ya Ziwa

Eneo Tarakimu Mfano wa msimbo wa kata
Mkoa wa Geita 30
Wilaya ya Geita 301 Kalangalala 30101
Wilaya ya Nyang'hwale 302 Nyang'hwale 30201
Wilaya ya Chato 303 Chato 30301
Wilaya ya Mbogwe 304 Iponya 30401
Wilaya ya Bukombe 305 Bukombe 30501
Mkoa wa Mara 31
Manisipaa ya Musoma 311 Mwigobero 31102
Wilaya ya Musoma 312 Murangi 31217
Wilaya ya Butiama 312 Makojo 31220
Wilaya ya Rorya 313 Bukura 31301
Wilaya ya Tarime 314 Bomani 31401
Wilaya ya Bunda 315 Bunda Mjini 31501
Wilaya ya Serengeti 316 Mugumu Mjini 31601
Mkoa wa Mwanza 33
Manisipaa ya Nyamagana 331 Nyamagana 33101
Manisipaa ya Ilemela 332 Nyakato 33201
Wilaya ya Sengerema 333 Ibisabageni 33301
Wilaya ya Magu 334 Magu mjini 33401
Wilaya ya Misungwi 335 Nhundulu 33501
Wilaya ya Ukerewe 336 Nansio 33601
Wilaya ya Kwimba 338 Ngudu 33801
Mkoa wa Kagera 35
Manisipaa ya Bukoba 351 Bakoba 35101
Wilaya ya Bukoba Vijijini 352 Buhendangabo 35201
Wilaya ya Missenyi 353 Ishozi 35301
Wilaya ya Karagwe 354 Kayanga 35402
Wilaya ya Muleba 355 Rushwa 35502
Wilaya ya Biharamulo 356 Biharamulo Mjini 35601
Wilaya ya Ngara 357 Ngara Mjini 35701
Wilaya ya Kyerwa 358 Kyerwa 35801
Mkoa wa Shinyanga 37
Manisipaa ya Shinyanga 371
Wilaya ya Shinyanga Vijijini 372
Wilaya ya Kahama 373 37311 Bugarama
Mji wa Kahama 373 Majengo 37301
Wilaya ya Kishapu 375 Kishapu 37501
Mkoa wa Simiyu 39
Wilaya ya Bariadi 391 Bariadi 39101
Wilaya ya Itilima 392 Lagangabilili 39201
Wilaya ya Maswa 393 BuchambiI 39301
Wilaya ya Meatu 394 Lubiga 39401
Wilaya ya Busega 395 Kabita 39501

4. Kanda ya Kati

Eneo Tarakimu Mfano wa msimbo wa kata
Mkoa wa Dodoma 41
Manisipaa ya Dodoma 411 ,

412

Tambukareli  41104 

Makutopora 41201

Wilaya ya Bahi 413 Bahi 41301 Bahi Sokoni
Wilaya ya Chamwino 414 Chilonwa 41401
Wilaya ya Kongwa 415 Kongwa 41501
Wilaya ya Mpwapwa 416 Mpwapwa mjini 41601
Wilaya ya Kondoa 417 Kondoa mjini 41701
Wilaya ya Chemba 418 Chemba 41801
Mkoa wa Singida 43
Manisipaa ya Singida 431
Wilaya ya Singida Vijijini 432
Wilaya ya Iramba 433 Kiomboi 43301
Wilaya ya Manyoni 434 Manyoni Urban 43401
Wilaya ya Mkalama 435 Kinyangiri 43501
Wilaya ya Ikungi 436 Ihanja 43601
Mkoa wa Tabora 45
Manisipaa ya Tabora 451
Wilaya ya Uyui 452 Goweko 45201
Wilaya ya Sikonge 453 Sikonge 45301
Wilaya ya Nzega 454 Nzega mjini 45401
Wilaya ya Urambo 455 Urambo 45501
Wilaya ya Igunga 456 Igunga 45601
Wilaya ya Kaliua 457 Kaliua 45701
Mkoa wa Kigoma 47
Manisipaa ya Kigoma-Ujiji 471
Wilaya ya Kigoma Vijijini 472
Mji wa Kasulu 473
Wilaya ya Kasulu 473 Kasulu Mjini 47301
Wilaya ya Kibondo 474 Kibondo Mjini 47401
Wilaya ya Buhigwe 475 Buhigwe 47501
Wilaya ya Uvinza 476 Uvinza 47601
Wilaya ya Kakonko 477 Nyabibuye  47709 

5. Kanda ya Nyanda za Juu Kusini

Eneo Tarakimu Mfano wa msimbo wa kata
Mkoa wa Katavi 50
Mji wa Mpanda 501
Wilaya ya Tanganyika 502 Ikola  50203 
Wilaya ya Mlele 503 Inyonga 50301
Mkoa wa Iringa 51
Manisipaa ya Iringa 511
Wilaya ya Iringa Vijijini 512
Wilaya ya Kilolo 513 Irole 51301
Mji wa Mafinga 514 Boma/Mafinga 51401
Wilaya ya Mufindi 514
Mkoa wa Mbeya 53
Mji wa Mbeya 531
Wilaya ya Mbeya Vijijini 532
Wilaya ya Rungwe 535 Bulyaga 53501
Wilaya ya Mbarali 536 Rujewa 53601
Wilaya ya Kyela 537 Kyela mjini 53701
Wilaya ya Chunya 538
Mkoa wa Songwe 54
Wilaya ya Songwe 541
Wilaya ya Mbozi 542
Wilaya ya Ileje 543
Wilaya ya Momba 544
Mji wa Tunduma 544
Mkoa wa Rukwa 55
Manisipaa ya Sumbawanga 551 Izia  55102 
Wilaya ya Sumbawanga Vijijini 552
Wilaya ya Nkasi 553 Namanyere 55301
Wilaya ya Kalambo 554 Matai 55401
Mkoa wa Ruvuma 57
Manisipaa ya Songea 571 Misufini  57102 
Wilaya ya Songea Vijijini 572
Wilaya ya Namtumbo 573 Namtumbo 57301
Wilaya ya Mbinga 574 Mbinga Mjini 57401
Wilaya ya Nyasa 575 Mbambabay 57501
Wilaya ya Tunduru 576
Mkoa wa Njombe 59
Mji wa Njombe 591 Njombe Mjini 59101
Wilaya ya Njombe Vijijini 592
Mji wa Makambako 592
Wilaya ya Wanging'ombe 593 Mdandu 59301
Wilaya ya Ludewa 594 Ludewa 59401
Wilaya ya Makete 595 Iwawa 59501

6. Kanda ya Pwani

Eneo Tarakimu Mfano wa msimbo wa kata
Mkoa wa Pwani 61
Mji wa Kibaha 611 Mailimoja 61102
Wilaya ya Kibaha 612 Mlandizi 61201
Wilaya ya Bagamoyo 613 Yombo 61306
Wilaya ya Kisarawe 614
Wilaya ya Mkuranga 615 Kiparang'anda 61502
Wilaya ya Rufiji
Wilaya ya Kibiti
616 Utete 61601
Kibiti 61610
Wilaya ya Mafia 617
Mkoa wa Mtwara 63
Manisipaa ya Mtwara 631
Wilaya ya Mtwara 632
Wilaya ya Tandahimba 633
Wilaya ya Newala 634
Wilaya ya Masasi 635 Mwenge Mtapika 63529
Wilaya ya Nanyumbu 636 Nangomba  63601 
Mkoa wa Lindi 65
Manisipaa ya Lindi 651 Makonde 65101
Wilaya ya Lindi 652 Nachunyu 65201
Wilaya ya Nachingwea 653
Wilaya ya Kilwa 654 Kilwa Masoko 65401
Wilaya ya Liwale 655 Liwale Mjini 65501
Wilaya ya Ruangwa 656 Ruangwa 65601
Mkoa wa Morogoro 67
Manisipaa ya Morogoro 671
Wilaya ya Morogoro 672
Wilaya ya Mvomero 673
Wilaya ya Kilosa 674
Wilaya ya Kilombero 675
Wilaya ya Ulanga 676 Mahenge 67601
Wilaya ya Gairo 677 Gairo 67701

7. Kanda ya Zanzibar

Eneo Tarakimu Mfano wa msimbo wa kata
Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja 71
Wilaya ya Mjini 711
Wilaya ya Magharibi Unguja 712 Mwanakwerekwe 71201
Mkoa wa Kusini Unguja 72
Wilaya ya Kusini 721
Wilaya ya Kati 722 Dunga 72201
Mkoa wa Kaskazini Unguja 73
Wilaya ya Kaskazini A 731
Wilaya ya Kaskazini B 732 Mahonda 73201
Mkoa wa Kusini Pemba 74
Wilaya ya Mkoani 741
Wilaya ya Chake Chake 742 Chanjaani 74201
Mkoa wa Kaskazini Pemba 75
Wilaya ya Wete 751
Wilaya ya Micheweni 752 Micheweni 75201

Tanbihi

  1. Kwa mfano wilaya za Handeni mjini na vijijini ziko pamoja chini ya na. 218; ilhali kila kata ya wilaya ya Handeni vijijini ina msimbo wa posta, upande wa mjini kuna misimbo 3 pekee ilhali kata za mjini ziko 12.

Viungo vya Nje