Mkoa wa Kagera

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mkoa wa Kagera
Nembo ya Tanzania
Nembo ya Tanzania
Mahali pa Mkoa wa Kagera katika Tanzania
Mahali pa Mkoa wa Kagera katika Tanzania
Anwani ya kijiografia: 1°55′S 31°18′E / 1.917°S 31.3°E / -1.917; 31.3
Nchi Tanzania
Wilaya 8
Mji mkuu Bukoba
Serikali
 - Mkuu wa Mkoa Mohamed Babu
Eneo
 - Mkoa 40,838 km²
 - Bara 28,953 km² 
 - Maji 11,885 km² 
Idadi ya wakazi (2002)
 - 2,003,888
Tovuti: http://www.kagera.go.tz/

Mkoa wa Kagera ni mkoa wa kaskazini-magharibi kabisa katika Tanzania. Jina lake linatokana na mto Kagera.

Mkoa wa Kagera umepakana na Burundi, Rwanda na Uganda upande wa Magharibi na Kaskazini. Upande wa Kusini umepakana na mikoa mengine ya Tanzania ya Kigoma, Shinyanga na Mwanza. Eneo lake ni 28,953 km² za nchi kavu na 11,885 km² za maji hasa ya Viktoria Nyanza, jumla 40,838 km².

Mkoa wa Kagera uko mnamo 1000 m juu ya uwiano wa bahari.

Makao makuu ya mkoa ni mji wa Bukoba.

Kuna wilaya saba za Bukoba Mjini, Bukoba Vijijini, Misenyi, Muleba, Karagwe, Ngara, Biharamulo na Kyerwa. Misenyi ni wilaya mpya iliyoanzishwa mwaka 2007 na Kyerwa ikafuata mwaka 2012.

Sensa ya mwaka 2002 imeonyesha idadi ya wakazi kuwa 2,003,888 inayoendelea kuongezeka asilimia 3.1% kwa mwaka.

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Katika mkoa huu elimu kama elimu bado haijaendelea kwa watu wote walioko vijijini hali hiyo hufanya taifa kurudi nyuma kimaendeleo maana taifa kama taifa huongozwa na wasomi ili kukua kiuchumi.

Majimbo ya bunge[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

External links[hariri | hariri chanzo]


 
Mikoa ya Tanzania
Bandera Tanzania
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Songwe | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi